Tuesday, July 23, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA LUCY KOMBA KUHUSU NDIKUMANA, WAIGIZA PAMOJA FILAMU YA KWANINI NISIMUOE.



Lucy Komba na Hamad Ndikumana
Muigizaji maarufu Swahiliwood Lucy Komba amemsifia Hamad Ndikumana(Kataut) ambaye ameigiza nae katika filamu mpya ya "Kwanini Nisimuoe" kuwa ana kipaji cha uigizaji tofauti na alivyofikiria mwanzoni kuwa inaweza kuwa shida kidogo wakati alipomfuata kwa ajili ya utengenezaji wa filamu hiyo. Ndikumana ni msakata kambumbu maarufu akiwa mwenyeji wa Rwanda na alimuoa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya miaka michache iliyopita ingawa kwasasa wanadaiwa kutengana.

Akichonga na Swahiliworldplanet kutokea nchini Denmark alipo sasa Lucy Komba alisema "Ndiku ana kipaji kusema ukweli wakati namchukua kufanya nae kazi nilijua nitapata nae tabu sana lakini ni tofauti na nilivyofikiria ni mtu mmoja kichwa sana yaani msanii ni msanii tu alicheza mpaka mwenyewe nilifurahi kwa kifupi ana kipaji cha uigizaji, maelekezo kweli nilimpa na kumfundisha nilimfundisha lakini uchezaji wake ulikuwa juu zaidi"

Lucy Komba ameibua waigizaji wengi maarufu wanaotamba sasa wakiwemo Jackline Wolper, Mzee Chillo na Irene Uwoya hivyo usije kushangaa Ndiku akifanya kweli kwenye kiwanda cha filamu. Filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni muda sio mrefu

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...