KWA wiki moja sasa, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti
kwamba, kujisikia kizunguzungu hatimaye kuanguka na kupoteza fahamu
kulikomtokea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
wakati akihojiwa na polisi kulitokana na kuulizwa maswali yaliyohusu
namna alivyozipata mali zake.
Machi 28, mwaka huu Mchungaji Gwajima alipojisalimisha Kituo Kikuu
cha Polisi Kanda Maaalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kumtolea maneno
yenye kuudhi Askofu wa Kanisa la Romani Katoliki Jimbo Kuu la Dar,
Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, alijikuta akizidiwa ghafla na
kukimbizwa Hospitali ya TMJ kwa matibabu huku akiwa amepoteza fahamu.
Ilidaiwa kuwa, Gwajima alipokwenda kituoni hapo kujisalimisha
alitarajia kukutana na mahojiano ya kuhusu kauli yake ya kumkashifu
Kadinali Pengo, lakini matokeo yake akakumbana na maswali ya kuhusu mali
zake.
WALIVYOSEMA WATU
“Unajua Gwajima yeye alipoambiwa ajisalimishe
Central kwa kumkashifu Pengo alijua akifika pale ataulizwa kwa nini
ulimtusi Pengo? Alikukosea nini? Huoni kama yule ni mtu mzima kuliko
wewe? Je, uko tayari kumwomba radhi? Lakini matokeo yake katikati ya
maswali akaulizwa mali alizonazo alizipata kwa njia gani?”
KWA NINI ALIZIMIA SASA?
“Sasa suala siyo kwamba swali hilo la kuhusu mali lilikuwa na shida
kwake, bali lilikuwa la ghafla ndiyo maana akajikuta akichanganyikiwa na
kupoteza fahamu,” kilisema chanzo kimoja.“Wengi wanasema alipoulizwa
kuhusu mali alizimia kwa sababu mali zenyewe si halali, hapana! Zile
mali ni halali kabisa ila swali halikuwa kwenye mawazo ya Gwajima,”
kiliendelea kusema chanzo.
Friday, April 3, 2015
RAY AMSALITI CHUCHU KWA HUSNA, WANASWA USIKU
Musa mateja
MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, amedaiwa kumsaliti mpenzi wake wa siku nyingi, Chuchu Hans baada ya kukutwa akiwa amepozi kimahaba na mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2011, Husna Maulid katika Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar, hivi karibuni.
Muigizaji nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akipozi kimahaba na Husna Maulid.
Wawili hao waliokuwa wamepakatana, walikutwa katika ukumbi huo wakati bendi mbili kubwa za muziki wa dansi nchini, FM Academia na The African Stars ‘Twanga Pepeta’ zilipokuwa zikiangusha burudani kabambe ya kushindana.
Uwepo wa Ray na Husna ulitafsiriwa kuwa ni usaliti kwani muda wote waliokuwa ndani ya ukumbi huo wawili hao walikuwa wamegandana kimahaba huku wataalamu wa ubuyu wakikazia madai kwa kusema wawili hao ni wapenzi.
“Sasa wewe kusoma hujui hata picha huoni? Hawa watakuwa ni wapenzi tu, haiwezekani mtu mpakatane, mpeane kampani kiasi hiki na mtu ambaye siyo mtu wako,” alisikika shuhuda mmoja.
Ray ambaye kabla ya kuwa na Chuchu aliwahi kutoka kimapenzi na mwigizaji Blandina Changula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, alionekana kufurahia kumpakata Husna huku wakipeana kampani ya kuzungumza, lakini alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa akifuatiliwa na kamera ya paparazi wetu.
Kutokana na mazingira ya wawili hao ukumbini hapo, paparazi wetu alishindwa kuzungumza nao juu ya ishu hiyo na hata alipowatafuta kwa simu siku iliyofuata, simu zao ziliita bila kupokelewa (huenda walijua wataulizwa nini).Lakini Chuchu, ambaye ndiye ‘mmiliki’ wa Ray hivi sasa, alipoulizwa kama anajua lolote juu ya ukaribu wa watu hao, alishtuka na kudai haamini kama Ray anaweza kumsaliti au amewahi kupiga picha na Husna za kimahaba.
“Khaa! Unasemaje? Mimi siamini labda kama kuna picha zao za pamoja naomba unitumie Whatsapp nizione maana nashindwa niongee nini, sikujua kama walienda popote Ray na Husna.”
Mwanahabari wetu alimtumia picha hizo Chuchu lakini hadi tunakwenda mitamboni, mrembo huyo hakuwa amejibu kitu chochote.

Thursday, April 2, 2015
YOUNG KILLER AKANA DEMU WAKE KUWA CHINI YA 18
MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, Erick Msodoki ‘Young Killer’
amekanusha madai kuwa demu wake anayejulikana kwa jina la Halimaty ana
miaka chini ya 18.Akipiga stori na Ijumaa kuhusiana na ishu hiyo, Young
Killer anashangaa watu kudai demu wake huyo ni ‘under age’ wakati ukweli
ana miaka 20.
“Mpenzi wangu ana miaka 20 na siyo kwamba eti nimemchukua kihuni tu mtaani, hapana! Nimempata kwa ridhaa ya wazazi wake sasa nashangaa hizo tuhuma zinatokea wapi,” alisema Young Killer

WEMA AKATAA UNAFIKI, AMPONGEZA CHIBU
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza
na kusema kuwa hata yeye anampa pongezi mpenzi wake wa zamani, Nasibu
Abdul ‘Diamond’ kwa jitihada alizozifanya mpaka kufikia hatua ya
kumaliza nyumba yake iliyopo Madale jijini Dar.
Akizungumza juzi, Wema alisema kuwa hata kama hawako pamoja lakini kama kuna kitu cha kumsifia kwa jambo zuri alilofanya hana sababu ya kukaa kimya na akinyamaza atakuwa mnafiki.
“Nikikaa kimya bila ya kumpongeza Chibu nitakuwa mnafiki, amefanya jambo zuri la kuigwa hivyo binafsi nampongeza kwa hapo alipofikia,” alisema Wema ambaye katika hatua za mwanzo za ujenzi huo alishiriki.

Tuesday, March 31, 2015
WEMA, IDRIS MAHABA NIUE!
WAPENZI? Kwa mara nyingine Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu
amesababisha kichwa cha habari kufuatia kunaswa ‘live’ usiku mnene akiwa
na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan
wakioneshana vitendo vya ‘nakupenda tu’ mbele ya kadamnasi, Risasi
Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akiwa na mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
NI ESCAPE ONE MIKOCHENI
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Kutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.

Kitendo cha wawili hao kukaa karibu tu, fasta walianza kuongea kwa staili ya kunong’onezana kwa muda mrefu, wakati mwingine wakishikana mikono.Kuna wakati walikwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kupapasana mapajani huku wakiendelea kuzungumza maneno ambayo hayakuweza kusikika kwa sababu ya sauti ya muziki ukumbini hapo kuwa juu.
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
Baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kadhaa wawili hao, alimfuata Wema na kumuuliza ili kujua kama ameamua kujiweka ‘mazima’ kwa Idris au la! Wema alijibu kwa kifupi:“Bwana wee si kila unachokiona kinahitaji ufafanuzi, wewe si ushapiga picha inatosha, maswali ya nini sasa?”
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.
Stori imetayarishwa na Musa Mateja, Chande Abdallah na Deogratius Mongela.
Wawili hao walinaswa wakioneshana mahaba niue hayo usiku wa kuamkia Machi 29, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar walipokuwa wamekwenda kushuhudia shoo kali ya mpambano kati ya Bendi za The African Stars ‘Twanga Pepeta’ na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.
PICHA LILIVYOANZA
Awali, paparazi wetu aliyeamua kulivalia njuga tukio hilo alimshuhudia Wema akiingia ukumbini humo akiwa sanjari na kampani yake, akiwemo shosti wake mkubwa kwa sasa, Aunt Ezekiel na mshauri wake kikazi, Petit Man.
Walikwenda kukaa kwenye viti vilivyokaribiana na kuanza kufuatilia mpambano wa bendi hizo mbili kubwa nchini uliokuwa ukiendelea jukwaani kwa kishindo kikuu.
Idris akimweleza jambo Wema Sepetu.
PETIT AKAA NA MADAMKutokana na mpangilio wa watatu hao, Petit Man alikaa katikati ya Wema (kushoto kwake) na Aunt, lakini muda mwingi alikuwa akinong’onezana na Madam huyo huku wakionekana kuzungumza mawili matatu yahusuyo mpambano huo unavyoendelea.
IDRIS NDANI YA NYUMBA
Ndani ya dakika kama ishirini tangu Wema na msafara wake waingie ukumbini humo, Idris naye aliwasili akiwa ameongozana na mdogo wa hiari wa Wema aitwaye Bite pamoja na mtu mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Nao walikwenda walipokuwa wamekaa akina Wema.
ONA HII SASA
Kuonesha kwamba itifaki inazingatiwa, Idris alipofika mahali hapo, Petit alisogeza nyuma kiti chake na kuwafanya Wema na Idris waweze kukaribiana na kuzungumza kwa ujirani zaidi.
Wakipozi kimahaba.
WAANZA KUNONG’ONEZANAKitendo cha wawili hao kukaa karibu tu, fasta walianza kuongea kwa staili ya kunong’onezana kwa muda mrefu, wakati mwingine wakishikana mikono.Kuna wakati walikwenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kupapasana mapajani huku wakiendelea kuzungumza maneno ambayo hayakuweza kusikika kwa sababu ya sauti ya muziki ukumbini hapo kuwa juu.
WAFUTANA JASHO
Kama vile hiyo haitoshi, ilifika mahali Wema alionekana usoni kuvuja jasho kwa mbali, basi alichukua skafu ya Idris kutoka shingoni na kujifuta ambapo Idris naye alimsaidia na baadaye Wema naye alifanya vivyo hivyo pale mwenzake huyo naye alipotokwa na jasho.
“Mh! Mwenzangu we acha tu. Hii ndiyo inaonesha sasa Wema na Idris kuna kitu, maana siku za hivi karibuni, kila alipokuwa anakwenda Wema, Idris naye alikuwa hakosi sasa leo hapa ndiyo full mahaba niue, hatari,” alisikika mpenda ‘ubuyu’ mmoja.
PICHA ZINAJIELEZA?
Baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha kadhaa wawili hao, alimfuata Wema na kumuuliza ili kujua kama ameamua kujiweka ‘mazima’ kwa Idris au la! Wema alijibu kwa kifupi:“Bwana wee si kila unachokiona kinahitaji ufafanuzi, wewe si ushapiga picha inatosha, maswali ya nini sasa?”
IDRIS AGOMA KUZUNGUMZA
Jitihada za kuzungumza na Idris ziligonga mwamba kutokana na staa huyo wa BBA aliyejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani laki tatu (zaidi sh mil. 514) kutokuwa tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ukaribu wake na Wema ukumbini hapo.
MUDA WA KUONDOKA WAFIKA, WAONDOKA PAMOJA
Wakati shoo ikielekea ukingoni, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiongozana katika msafara mmoja na Aunt, Petit na Bite ambapo walitokomea kusikojulikana.
Stori imetayarishwa na Musa Mateja, Chande Abdallah na Deogratius Mongela.
Subscribe to:
Posts (Atom)