Wednesday, January 20, 2016

SIMBA SC YAICHALAZA 2-0 JKT RUVU TAIFAkI

 
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Siamba SC wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa kwa njia ya penalti na mchezaji wa Kimataifa Hamisi KizzaKikicheza mchezo wake wa 15 kwenye ligi kuu Tanzania bara, kikosi cha Simba leo kimeifunga timu ya JKT Ruvu 0 – 2
Kikosi cha timu ya Simba kikicheza mchezo wake wa 15 kwenye ligi kuu Tanzania bara, jana kilifanikiwa kuifunga timu ya JKT Ruvu mabao 2-0
Magoli yote yalifungwa katika kipindi cha pili ambapo goli la kwanza lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa Hamisi Kizza katika dakika ya 51 baada ya mshambuliaji Danny Lyanga kufanyiwa madhambi ndani ya boksi la timu ya JKT, kwa ustadi mkubwa Hamis Kizza alifunga penati hiyo na kufikisha jumla ya magoli 10 tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2015/2016. Goli la pili lilifungwa na mshambuliaji Lyanga dakika ya 61 baada ya pasi nzuri iliyotoka kwa beki wa kulia Nimubona ikamfikia Mkude na kumpasia Danny Lyanga ambapo aliwatoka mabeki pamoja na kipa na kufunga goli. Mpaka kipenga cha mwisho kinapigwa JKT Ruvu 0 – 2 Simba.
Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na kocha wa Simba Jackson Mayanja na kusema “tumefurahia sana ushindi wa leo haikuwa mechi rahisi ilikuwa ni mechi yenye ushindani mkubwa sana lakini kikosi changu kimeweza kupambana na hatimaye kuondoka na pointi 3 muhimu, tunatoa shukrani kwa mashabiki wanaoendelea kujitokeza kushangilia timu yetu kwa ajili ya kuhakikisha tunaendelea kupata matokeo mazuri.
Simbaports.co.tz inawapongeza wachezaji na benchi lote la ufundi kwa kazi nzuri ya leo iliyoiwezesha timu kushinda.
Unataka kuwa wa kwanza kupata habari za klabu yako ya Simba tuma neno Simba kwenda namba 15460 utatumiwa ujumbe jibu “OK” nawe utakuwa umejiunga na huduma ya Simba News. Huduma itakayokuwezesha kupata habari za Simba popote ulipo kwa wateja wa Tigo na Vodacom.
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...