Sehemu zilimobomolewa nyumba za
wakazi wa bonde la Mkwajuni kufuatia kuwa eneo hatarishi wakati wa kipindi cha
mvua.
|
MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa
kuamkia leo umelifanya Bonde la Mto Msimbaji jijini Dar es Salaam, kufurika kwa
maji jambo ambalo limedhihilisha wazi kuwa sehemu hiyo ambayo hivi karibuni ilishuhudiwa nyumba kibao zikivunjwa ili kuokoa
wakazi wa sehemu kuendelea kupata aza ya kuingiliwa na maji ya mafuriko
hatimaye sasa imetoa ishara ya wazi kuwa
shehemu hiyo ni hatari kwa kufanywa
makazi ya binadamu.
Mwandishi wetu amefanikiwa
kufika eneo hilo na kujionea hali halisi ya maji yakijaa eneo hilo ambapo zilikuwepo nyumba za wakazi
wa sehemu hiyo ambao wamekuwa waking’ang’ania kuendelea kukaa eneo hilo
hatarishi.
Mamlaka zinazohusika na uangalizi wa hali ya hewa zimesema kuwa mvua zitaendelea kunyesha kwa
wingi katika kipindi hiki cha ukanda wa Pwani hivyo wananchi waishio mabondeni
wanatakiwa kuchukua tahadhali kubwa ili kuepusha maafa yasiyokuwa ya lazima.
Taswira ya Mto Msimbazi unaotiririsha maji yake katika bonde la Mkwajuni baada ya kunyesha mvua. |
Maji yakiwa yamefurika eneo zilimobomolewa nyumba kufuatia mvua ziliyoanza kunyesha usiku wa kuamkia leo Dar. |
Muonekano wa nyumba zilizosalia eneo hilo baada ya zilizokuwa bondeni kubomolewa.
|
Maji yakiwa yamejaa sehemu ya bonde ambapo nyumba zilivunjwa na serikali hivi karibuni. |
Baadhi ya vipande vya mbao
vilivyokuwa mapaa ya nyumba zilizo bondeni.
|
No comments:
Post a Comment