Tuesday, January 19, 2016

SOMA MANENO YA DOTNATA SIKU MBILI BAADA YA KUPATA AJALI NA KUVUNJIKA MFUPA!

Muigizaji na mwanamuziki wa siku nyingi Dotnata akishushwa kwenye gari la wagonjwa katika Hospitali ya  Taifa ya Muihimbili baada ya kupata ajali iliyompelekea kuvunjika mguu.
 HAYA NDIYO MANENO YA DOTNATA AKIWAHUSIA MARAFIKI ZAKE SOMA MWENYEWE:  Marafiki zangu nimewamis. Nimepatwa na mtihani wa kuvunjika mguu leo ni siku ya nne. Namshukuru Mungu kwa yote mimi nina pacha wangu siku ya Ijumaa nilipata ajali na kwa bahati mbaya nilivunjika mguu hivyo mfupa mkubwa wa paja ndiyo ulipata adha hiyo.

Mwenzangu naye alivamiwa na kundii la Panya road, majira ya saa kumi alfajiri, kwa sasa kila mtu yupo kwake yaani ni shida maana adha hii imetupata  siku  moja.

Kwa kifupi tu mimi nimelazwa Katika Hospital ya Muhimbili Moi,  mwenzangu yupo katika Hospitali ya Hindmandal, Najuwa shetani alijiinua, ila hatuna sababu ya kumshukuru na kumuomba Mungu atuepushe na kila lililo baya kwetu. 
 Pacha wa Dotnata akiwa Hospitali baada ya kuvamiwa na Panya Road ambao walimshambulia kiasi cha kujikuta akipoteza fahamu na kupelekwa katika Hospitali ya Hindmandal.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...