Tuesday, June 2, 2015

SHAMSA AONESHA JEURI KWA MZAZI MWENZAKE

STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana.
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.
Akistorisha  na gazeti hili Shamsa alisema tangu wamwagane na mzazi mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama yake bila baba.
“Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka? Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...