Tuesday, June 2, 2015

THEA ABARIKI MUMEWE KUOA

SHIDA! Baada ya ndoa yao kuvunjika, msanii mkongwe wa filamu, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka na kumbariki aliyekuwa mume wake, Michael Sangu ‘Mike’ kuoa kwani hana pingamizi.
Msanii mkongwe wa filamu, Salome Urassa ‘Thea’.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Thea alisema katika akili yake hana kumbukumbu kama aliwahi kuolewa na mwanaume huyo (ukweli walifunga ndoa 2010) na hataki kumzungumzia ila kama anataka kuoa aoe kwani hana shida naye na hana malalamiko yoyote.
Baada ya kumsikiliza mwanamama huyo, paparazi wetu alimtafuta Mike ambaye alisema; “Kutokana na Thea kuongea maneno ya kashfa na kudai kwamba hanijui, niko kwenye mazungumzo na familia na mke wangu wa kwanza, Ummy Mohamed ambaye tuna mtoto mmoja hivyo kama mambo yakienda vizuri  nitamrudia kwani namuona ni bora zaidi.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...