Mayasa Mariwata na Gladness Mallya
MAJANGA! Msanii wa
filamu Bongo, Fatuma Ayubu `Bozi’ amejikuta akifungasha virago na kuhama
kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kutokana
na mjengo huo kutawaliwa na mauzauza yanayosadikiwa kuwa ya
kishirikina.
Chanzo makini kilicho jirani na nyumba
aliyokuwa akiishi mwanadada huyo kilieleza kuwa, baada ya kuvumilia
vimbwanga vya kishirikina ameamua kuondoka.



“Kuna muda nikiwa chumbani nasikia taa
zinawashwa na kuzimwa nikitazama sioni mtu, wakati mwingine paka anakuja
chumbani na kucheza kwenye kioo ukimfukuza na kufunga mlango dakika
chache unamuona tena na cha kustaajabisha nakuwa najiuliza amepita wapi
sipati jibu, kwa ujumla nyumba hii ina mauzauza kibao ambayo nimeshindwa
kuyavumilia, hali ni mbaya nahamia kwa rafiki yangu,” alisema Bozi.
No comments:
Post a Comment