
Musa Mateja
MREMBO anayefanya poa
kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’
kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye
William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’
kiukoo.
Ndani ya Ukumbi wa Triple 7 uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni,
paparazi wetu aliwaona wakiingia sambamba na kukaa beneti kama mtu na
mpenzi wake jambo lililozua maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo
ukumbini hapo.



Ndani ya Triple 7, paparazi wetu aliamua
kumfuata Linah ili ajiridhishe uwepo wake na mwanaume huyo ambapo
msanii huyo alijing’atang’ata na kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa natoka naye.
Sijui umenielewa? Natoka naye sehemu mbalimbali.Ila kukutoa wasiwasi
tambua kwa sasa sina mpenzi na nina haki ya kuwa naye, sina mpaka wa
kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.
No comments:
Post a Comment