Thursday, June 25, 2015

VIFO MASTAA KUTIKISA UPYA!

MSHTUKO! Wakati wimbi la wasanii Bongo likizidi kuwa kubwa katika kutangaza nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye siasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein amefunguka mazito juu ya vifo vya mastaa hao kutikisa upya huku wale watakaosalia wakipata nafasi za uongozi.
steveveeStaa wa bongo movie Steven Mangele ‘Steve Nyerere’.
TUJIUNGE MAGOMENI-MWEMBECHAI
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Magomeni-Mwembechai jijini Dar, mapema wiki hii, mtabiri huyo alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wa mafanikio makubwa kwa wasanii lakini pia vifo navyo vitakuwa vingi kwao.
Wema-SepetuMiss tanzania 2006 na muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu.
NI MWAKA WAO KINYOTA
Alisema kwamba, kwa wale watakaosalimika huku wakiwa wamejiingiza kwenye kinyang’anyiro cha kugombea uongozi wa kisiasa, wote watafanikiwa kwa kuwa mwaka huu ni wao.
Maalim alisema kuwa, mwaka huu kinyota ni wao ndiyo maana wamejitokeza wengi kwenye kuwania nafasi hizo tofauti na vipindi vingine vya uchaguzi vilivyopita.

king-majutoMuigizaji mkongwe King Majuto.
“Mwaka huu kinyota ni wa mafanikio kwa wasanii lakini pamoja na kufanikiwa sana vifo navyo vitakuwa ni vingi mno, kwa hiyo wale wote waliojiingiza kwenye siasa watafanikiwa na watapata madaraka,” alisema mtabiri huyo.
WAFANYEJE KUKABILIANA NA VIFO?
Ili kukabiliana na jinamizi hilo la umauti, mtabiri huyo aliwataka mastaa kuwa watu wa ibada muda wote na kuachana na mambo ya starehe za kidunia.
“Usalama wao ni kuacha starehe. Hiyo ndiyo itakuwa njia sahihi ya kuepukana na roho wa vifo lakini kama hawatafanya hivyo, vifo vitakuwa vingi na vitawatikisa vilivyo,” alisema Maalim.
MASTAA WALIOTANGAZA NIA
Mpaka sasa mastaa wengi wameshatangaza nia ya kugombea nafasi za ubunge kupitia vyama mbalimbali vya siasa akiwemo, Wema Isaac Sepetu, Wastara Juma, Salome Urasa ‘Thea’, Aunt Fifii, wote Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wengine ni Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Amri Athuman ‘King Majuto’ kupitia tiketi ya CCM,  Seleman Msindi ‘Afande Sele’ kwa ‘leseni ya Chama cha  Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) na Joseph Haule ‘Profesa Jay’ kupitia Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema).
Kwa mujibu wa Maalim, mastaa hao anawatabiria kuwika na wengine kuibuka kidedea kwenye uchaguzi kwa kuwa nyota zao zinang’aa kwa mwaka huu.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kuliibuka upepo mbaya wa vifo vya mastaa wa tasnia mbalimbali kabla ya wimbi hilo kutulia hivi karibuni huku mtabiri huyo akionesha shaka kuwa kinyota ishu hiyo inaweza kuanza kutikisha upya kabla ya uchaguzi mkuu.
WANGEKUWEPO
Baadhi ya mastaa waliokuwa na nguvu ya ushawishi mkubwa kwa mashabiki wao ambao kama wangekuwa hai walikuwa na nafasi kubwa ya kupata uongozi kisiasa endapo wangegombea ni pamoja na  marehemu Steven Kanumba ‘The Great’, Adam Kuambiana, John Maganga, Rachel Haule na Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na wengine wengi ambao vifo vyao vilitikisa ulimwengu wa burudani Bongo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...