Gladness Mallya
BAADA ya uvumi kuzagaa mtaani kwamba mwanamuziki wa dansi,
Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia, Banza amesema amechoshwa
na watu kumuua sana.
Baada ya uvumi huo, ndugu zake wamesema watu waache kumuua kwa maneno kwani bado yupo hai.
Ndungu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Hamis, alisema uzushi wa
kifo cha Banza umewasumbua sana kwani watu mbalimbali walikuwa wakipiga
simu na wengine kufika nyumbani jambo ambalo lilimuumiza sana Banza
japokuwa anaumwa lakini akawa analalamika kwa nini watu wanamuua kwa
maneno na si mara moja kutokea.
“Jamani yupo hai japokuwa anaumwa lakini anaongea tatizo lipo kwenye
kusimama na kula, watu waache uzushi kwani wanamuumiza zaidi kwa uzushi
wao huo,” alisema Hamis.
No comments:
Post a Comment