Saturday, June 27, 2015

WEMA KUBADILI WANAUME CHANZO NI HIKI


1Wema Sepetu na Nangari.
Mwandishi wetu
IMEBAINIKA! Kufuatia tabia yake ya kubadili wanaume, mrembo asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Isaac Sepetu imefahamika kuwa chanzo cha yote ni kusumbuliwa na ugonjwa ujulikanao kitaalamu kwa jina la Sex Maniac.
Wema-na-Diamond (1)Wema Sepetu na Diamond.
Akizungumza na gazeti hili, mtaalam wa masuala ya utabiri na nyota, Maalim Hassan Yahya alisema kwamba suala la Wema kubadili wanaume kila mara si kulogwa bali anasumbuliwa na ugonjwa huo ambao mtu akiwa nao kila wakati anawaza mapenzi na raha yake ni kufanya tendo la ndoa.
wemanacharlesbabaWema Sepetu na Chaz Baba.
Maalim alidadavua kwamba, ugonjwa huo hautibiwa na dawa za hospitali kama magonjwa mengine ila kama mtu anahitaji kuondokana na tatizo hilo anatakiwa kumtafuta mwanasaikolojia ambaye mara kwa mara atakuwa anamjenga kwa ushauri hadi atakapoona amekuwa sawa kwa kuacha kuwaza mambo hayo.
TBT-Wema-na-KanumbaWema Sepetu na Steven Kanumba.
“Watu wanashindwa kuelewa, unakuta mtu anakuwa na wanaume wengi, anabadili kila mara alafu watu wanamsema bila kujua kwamba ni ugonjwa ambao mtu anajikuta akipenda ngono kila wakati na kwenye mawazo yake anatawaliwa na kutamani tendo la ndoa tu.
IMG_0131Wema Sepetu  na Bob Juniour.
“Lakini wapo wengine wanabadili mabwana maarufu ili nao wawe maarufu,” alisema Maalim.
WemaJumbeWema Sepetu na Jumbe.
Wema aliwahi kutoka kimapenzi na wanaume tofauti akiwemo, Herry Samir ‘Mr. Blue’, Khaleed Mohamed ‘TID’, marehemu Steven Kanumba, Yusuf Jumbe, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, CK na Nagari Kombo.
Jitihada za kumpata Wema ili kuzungumzia hali hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani na kukosekana nyumbani kwake hivyo jitihada zinaendelea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...