Tuesday, June 30, 2015
Wizkid alifanya makusudi kutokwenda tuzo za BET, ameusema ukweli hapa
Toka tuzo za BET 2015 zifanyike juzi jumapili ya tarehe 28 June baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Africa wamekuwa
wakijitokeza kueleza sababu za kwanini hawakutokea kwenye tuzo hizo
mwaka huu wakidai hawafurahishwi na kitendo cha TV hii kubwa ya burudani
Marekani BET kuwatenga wasanii wa Kiafrika na wasanii wengine wakubwa wakati wa utoaji wa tuzo.
Kwa sababu utaratibu ni kwamba Wasanii
wa Afrika hupewa tuzo yao asubuhi wakati Wasanii wakubwa wa Marekani
kama kina Beyonce na Chris Brown hupewa tuzo zao jioni kwenye tukio
lenyewe huku wakishuhudiwa na wageni waalikwa, tofauti na wa Afrika
ambao huwa hakuna mgeni hata mmoja kwenye ukumbi.
Monday, June 29, 2015
MO ASSURANCE YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATANZANIA MAONYESHO YA SABASABA

Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama ( wa pili kushoto) akiwa na timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watakaokua wanatoa huduma katika Banda la MO ASSURANCE lilipo ndani ya mabanda ya MeTL Group kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa wa kampuni ya MO ASSURANCE, Mariot Ndomba, Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack pamoja na Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MO ASSURANCE, Esther Moringi.
MO Assurance kampuni ya bima inayohudumia nchi nzima kwa kutoa huduma mbalimbali za bima za majanga ikiwemo ajali ya moto, bima ya wizi, bima za ajali mbalimbali.
“MO Assurance tunapatikana ndani ya jengo la CRDB gorofa ya nane, mtaa wa Azikiwe ambapo tunatoa huduma mbalimbali za bima.” alibainisha meneja masoko msaidizi, Esther Moringi.
WAJUE MASTAA WANANE WA NIGERIA WENYE MAJUMBA YA UKWELI

Hili ni jumba la mwigizaji Genevieve Nnaji ambalo alilinunua jijini Accra, Ghana. Jengo hilo lina thamani ya dola milioni nne (Sh. Bilioni 8.6) likiwa eneo la Achimota.

Daniella Okeke
Huu ni mjengo unaotisha wa Daniella Okeke ambao una thamani ya mamilioni.

Ini Edo
Haya ni makazi ya Ini Edo, mmoja wa nyota maarufu wa filamu nchini Nigeria ambako anaishi baada ya kuachana na mfanyabiashara Philip Ehiagwina. Mjengo huo una thamani ya Naira milioni 70 za Nigeria. Mrembo huyo anaishi humo na wadogo zake.

Haya ni makazi ya mwigizaji Wasiu Ayinde ambaye anamiliki majumba kadhaa jijini Lagos na mji wa nyumbani kwao huko Ijebu.
Mjengo huu unaoitwa ‘Omoojusagbola House’ ulimalizika kujengwa Machi 2012 wakati akiadhimisha mwaka wa 55 tangu kuzaliwa kwake. Ayinde ambaye anajulikana kama K1 pia ana nyumba jijini Ontario, Canada, ambako mke na watoto wake wanaishi.
TASWIRA ZA TUZO ZA BET 2015 NA ORODHA YA WASHINDI
Janet Jackson akiwa na tuzo yake.
Rihanna katika pozi na Floyd Mayweather.
Rappa Nicki Minaj (kushoto) akiwa na Meek Mill.
Modo Blac Chyna (kushoto) akiwa na Amber Rose.
Karrueche Tran katika pozi.
Ciara.
Nicki Minaj.
Serayah.
Russell Wilson.
Kelly Rowland.
Brandy.
Ifuatayo ni orodha ya washindi
wa Tuzo za BET 2015 zilizofanyika jana kwenye Ukumbi wa Microsoft Los
Angeles, California nchini Marekani.Ultimate Icon, Music Dance Visual Award: Janet Jackson
Humanitarian Award: Tom Joyner
Best New Artist: Sam Smith
Best Female Hip-Hop Artist: Nicki Minaj
Best Male Hip-Hop Artist: Kendrick Lamar
Best Female R&B/Pop Artist: Beyoncé
Best Male R&B/Pop Artist: Chris Brown
Best International Act UK: Stormzy
Best International Act Africa: Stonebwoy
Best Group: Rae Sremmurd
Best Collaboration: Common & John Legend, "Glory"
Best Actress: Taraji P. Henson
Best Actor: Terrence Howard
Youngstars Award: Mo'ne Davis
Best Movie: Selma
Best Gospel Artist: Lecrae
Video of the Year: Beyoncé, "7/11"
Video Director of the Year: Beyoncé, Ed Burke & Todd Tourso
Sportswoman of the Year: Serena Williams
Sportsman of the Year: Stephen Curry
Coca-Cola Viewers' Choice Award: Nicki Minaj f/ Drake, Lil' Wayne & Chris Brown, "Only"
Centric Award: The Weeknd, "Earned It"
Fandemonium Award: Chris Brown
Lifetime Achievement Award: Smokey Robinson
Sunday, June 28, 2015
DIAMOND ATAITIWA AIRPORT DIAMOND KWA SAA MBILI
KIBANO! Staa wa Bongo Fleva mwenye jina kubwa Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya ‘kutaitiwa’ kwa saa mbili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kisa kikiwa wingi wa mabegi (3) makubwa aliyoshuka nayo akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Ijumaa Wikienda linakupa ‘unyunyuz’ kamili.
Tukio hilo lililoshuhudiwa hatua kwa hatua na gazeti hili, lilijiri Juni 26, mwaka huu kwenye eneo la kukagulia mizigo ya abiria uwanjani hapo kitendo kilichosababisha Diamond kutokwa na kijasho chembamba.
TAFSIRI YA MABEGI MAKUBWA
Chanzo chetu kilichokuwa ndani ya jengo la kutokea abiria kililiambia Ijumaa Wikienda kuwa, maafisa ukaguzi wa uwanja huo walimtilia shaka Diamond hivyo ikawalazimu wayakague mabegi hayo hadi ndani lakini pia walimkuta ana upungufu wa stakabadhi za mizigo hiyo.
KUHUSU STAKABADHI
Kuhusu stakabadhi zisizokuwepo, ilibidi Diamond ampigie simu ‘mdogo wake’ (si wa tumbo moja) aliyejulikana kwa jina la Q-Boy ampelekee kwani alitua nazo Bongo siku moja kabla, yaani Juni 25.
NDANI YA MABEGI
Ndani ya mabegi hayo, kulikutwa kamera, maiki na vifaa vya studio.

Shuhuda mmoja ambaye Ijumaa Wikienda lilimkuta nje ya chumba ambacho Diamond alikuwa akipekuliwa, alisema maafisa hao waliamini msanii huyo alikuwa ameshuka na madawa ya kulevya ‘unga’.“Unajua mastaa siku hizi wanaongoza kwa kubeba unga. Sasa serikali iko makini nao sana. Ndiyo maana wengi wao wakipita hapa wanakaguliwa kuliko abiria wengine,” alisema mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni dereva wa teksi uwanjani hapo.
DIAMOND APIGWA PICHA, AONGEA NA WIKIENDA
Paparazi wetu aliendelea kuganda mlangoni hapo hadi Diamond alipotoka na kumfotoa picha mbalimbali na baadaye alimfuata hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus na kumuuliza kama anajua kisa cha kupekuliwa kwa muda mrefu vile.
“Nilikuwa na mizigo naishughulikia ili itoke hivyo kuna mambo pia tulikuwa tunapishanapishana pale maana walihitaji nilipie ushuru wakati vifaa vya studio tulishaambiwa ni ‘free’ (bure). Pia kulikuwa na risiti za mizigo ambazo zilikuwa hazionekani, kumbe Q-Boy alitangulia nazo jana mimi nikawa nimesahau.
“Ila wao walikuwa wakijiridhisha kwenye mizigo yangu. Walifikiri nimebeba unga,” alisema Diamond.
HALI YA SASA UWANJANI
Mbali na Diamond kupekuliwa kwa muda mrefu, kwa sasa abiria wanaoingia na kutoka kwenye uwanja huo wamekuwa wakikaguliwa kwa umakini ili kubaini uhalali wa mizigo yao lengo kubwa ni kudhibiti uingiaji au utokaji wa madawa ya kulevya ambapo serikali imeweka umakini katika kupambana na biashara hiyo haramu.
CHRISTIAN BELLA
Ukiachana na Diamond, mastaa wengine waliowahi kukumbana na pekuapekua kama hiyo ni Mkurugenzi wa Bendi ya Malaika, Christian Bella na mtangazaji wa Radio Time FM, Hadija Shaibu ‘Dida’.
Bella yeye alikumbwa na adha hiyo, mwaka juzi, usiku wa saa nane akiwa anatokea nchini Uturuki na Ndege ya Shirika la Turkish Airways.
Dida naye ilikuwa mwaka 2012 ambapo alikumbwa na pekuapekua hiyo alipoingia uwanjani hapo kuelekea nchini Thailand kwa shughuli za kibiashara.
KANYE WEST AFANYA KWELI TAMASHA LA GLASTONBURY, AVAMIWA NA NJEMBA STEJINI
Saturday, June 27, 2015
RAIS KIKWETE KATIKA HAFLA YA MIAKA MIWILI YA KUTAWAZWA KWA POPE FRANCIS KUWA KULIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Vatican
na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla
kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis
kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya
balozi huyo jijini Dar es salaam
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania,
Francisco Montecillo Padilla qkihutubia kwenye sherehe za kuadhimisha
miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki
nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Mabalozi na viongozi mbalimbali kwenye sherehe za
kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa
kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini
Dar es salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe
Bernard Membe akiongea kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya
kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana
jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Sehemu ya maaskofu kwenye sherehe za kuadhimisha miaka
miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini
jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akisoma hotuba yake kwenye sherehe za
kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa
kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini
Dar es salaam
Rais Kikwete akigonganisha glasi na Balozi wa Vatican na
Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla na
Muadhama kardinali Polycarp Pengo kwenye sherehe za kuadhimisha miaka
miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa Katoliki
duniani jana jioni kwenye makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akigonganisha glasi na Kiongozi wa Mabalozi
nchini na Balozi wa DRC Mhe. Asumani Mpango pamoja na Mhe Membe na Rais
wa baraza la Maskofo wa Kikatoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa
Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye
makazi ya balozi huyo jijini Dar es salaam
Meza Kuu ikishereherekea miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki duniani
Meza Kuu wakati wa hafla hiyo
Rais Kikwete akiongea na Mabalozi na viongozi wengine
kwenye sherehe za kuadhimisha miaka miwili ya kutawazwa Papa Francis
kuwa Kiongozi wa kanisa katoliki nchini jana jioni kwenye makazi ya
balozi huyo jijini Dar es salaam
Waziri Membe akimtambulisha Balozi wa Vatican na Mwakilishi
wa Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla kwa Kaimu Mufti
wa Tanzania Sheikh abubakar Zubeiry aliyealikwa kwenye sherehe hizo
CHAMA CHA WAFANYAKAZI MADEREVA TANZANIA (TADWU), CHAMKABIDHI MLEZI WAO MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA RASIMU YA MKATABA WA MABORESHO YA MASLAHI YAO
Mlezi wa chama cha wafanyakazi madereva Tanzania (TADWU), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na madereva kabla ya kukabidhiwa rasimu ya maboresho ya maslahi ya madereva hao na cheti cha utambulisho wa chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara na Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, rasimu ya mkataba wa maslahi ya madereva waliyokuwa wakiidai serikali kwa muda mrefu Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda cheti cha utambulisho wa chama chao kipya kitakachoitwa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) baada kuundwa rasmi ambacho kitazindulia Julai Mosi mwaka huu.
Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said (kulia) akizungumzia yaliyomo kwenye rasimu hiyo na maboresho ya maslahi yao.
DC Makonda akisalimiana na madereva baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Madereva wakiwa wamesimama wakisubiri kusalimiana na mlezi wao DC Paul Makonda.
Ni usikivu kwa mlezi wao wakati akihutubia.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa madereva hao.
Madereva wakiwa kwenye mkutano huo.
Madereva wakishangilia hutuba ya mlezi wao Paul Makonda.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Madereva nchini nchini kimemkabidhi mlezi wao Mkuu wa Wlaya ya Kinondoni Paul Makonda rasimu ya mkataba uliobeba maboresha ya maslahi waliokuwa wanaidai kutoka kwa wamiliki pamoja na Serikali.
Katika hatua nyingine madereva hao Julai Mosi mwaka huu wanatarajiwa kuzindua chama chao ambacho kitaitwa Chama cha Madereva Wafanyakazi Tanzania (TADWU).
Hatua ya kutengeneza rasmu hiyo hiyo imekuja baada ya kikao walichokaa Juni 21 mwaka huu ambapo lengo lilikuwa ni kuwashinikiza waajiri kuwapa mikataba ya kudumu wakiwa kazini ikiwa ni pamoja na likizo za uzazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said alisema rasimu ya mkataba huo imebeba maboresho ya maslahi yao waliyokuwa wanadai.
Alisema madai hayo ni pamoja na bima ya maisha , mazishi yenye staha, muda wa kazi kisheria, matibabu, na nauli ya kwenda kazini.
"Leo tuna chama cha wafanyakazi madereva Tanzania , pia tumepewa mkataba hivyo nawatangazia madereva wote kuwa tumepata chombo cha kuzungumzia tofauti na ilivyokuwa awali.
Kwa sasa imebaki kujadili na serikali kuhusu kuboreshwa kwa mishahara hivyo napenda kuwatangazia madereva kuwa tumepata mikataba tuliyohitaji miaka mingi,"alisema.
Katibu huyo aliongeza kuwa chama hicho hakitasita kumchulia hatua za kisheria mmiliki atakayekiuka sheria hizo na kuongeza hakitasitakumpeleka kwenye vyombo vya sheria kama walivyokuwa wanawafanyia mwanzoni.
Akikabidhiwa mkataba huo kwa chama hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema mahali walipofikia madereva hao kwa sasa ni jambo la kuleta maendele makubwa.
Alisema watanzania wanatakiwa kutambua kuwa madai hayo si kwa ajili ya madereva peke yao bali ni kwa ajili ya taifa zima na kwamba kutatuliwa kwa changamoto hiyo kutapunguza ajali zinazoendelea kutokea nchini.
Makonda alisema asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipata ajali kutokana na kuchoka hivyo wanaposinzia usahau kuwa wanaendesha vyombo vya moto hivyo kusababisha ajali.
Katika hatua nyingine Makonda alisema kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari hawana mikataba ya kudumu na kwamba ni changamoto hivyo aliwataka kwenda kuonana nae ili kupata ushauri wa namna ya kuwawezesha kuhakikisha wanapewa mikataba ya ajira na waajiri wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Subscribe to:
Posts (Atom)