
Komediani wa Uingereza, Lee Nelson baada ya kupanda stejini kumpa sapoti Kanye West.
RAPPA wa nchini Marekani, Kanye West amefanya kweli kwa kuangusha
bonge la shoo katika Tamasha la Glastonbury nchini England jana usiku.
Mashabiki wakifuatilia burudani kutoka kwa Kanye West.
Mkali huyo alizikonga vilivyo nyoyo za mashabiki mbali na watu zaidi
ya 134,000 kupinga uteuzi wa jina lake kuwemo kwenye orodha ya watu
waliopanga kutumbuiza katika tamasha hilo wakitaka aondolewe na iwekwe
Bendi ya Muziki wa Rock huku mwandaaji wa tamasha hilo, Emily Eavis
akipokea vitisho vya kuuawa kupitia Twitter kwa uamuzi wa kumualika
West.
Kanye akizidi kufanya yake.

Mke wa Kanye, Kim Kardashian akichukua picha wakati mumewe akiwa stejini.
Shoo hiyo ya West, iliingiliwa na komediani raia wa Uingereza aitwaye
Lee Nelson aliyepanda stejini kumpa sapoti staa huyo kabla ya kushushwa
na wanausalama.
Kanye na Kim wakati wakiwasili Glastonbury tayari kwa shoo.
No comments:
Post a Comment