Toka tuzo za BET 2015 zifanyike juzi jumapili ya tarehe 28 June baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Africa wamekuwa
wakijitokeza kueleza sababu za kwanini hawakutokea kwenye tuzo hizo
mwaka huu wakidai hawafurahishwi na kitendo cha TV hii kubwa ya burudani
Marekani BET kuwatenga wasanii wa Kiafrika na wasanii wengine wakubwa wakati wa utoaji wa tuzo.
Kwa sababu utaratibu ni kwamba Wasanii
wa Afrika hupewa tuzo yao asubuhi wakati Wasanii wakubwa wa Marekani
kama kina Beyonce na Chris Brown hupewa tuzo zao jioni kwenye tukio
lenyewe huku wakishuhudiwa na wageni waalikwa, tofauti na wa Afrika
ambao huwa hakuna mgeni hata mmoja kwenye ukumbi.

Hii
picha ni wakati Davido wa Nigeria akipokea tuzo 2014, wanasema hata
nyuso zao zilikua zinaonyesha hawana furaha kihivyo sababu waliitwa
ukumbini asubuhi kabla ya tukio lenyewe jioni.
Jana msanii Fuse ODG ndio alitangaza
kwamba hakwenda kwenye utoaji wa tuzo hizo sababu Wasanii wa Afrika
wanadharaulika na kupewa tuzo backstage, saa kadhaa zilizopita aliefatia
kwenye headlines ni Wizkid wa Nigeria anaesema hatokwenda kwenye hizi
tuzo hizo kama BET wataendelea kuwapa wasanii wa Kiafrica tuzo zao nyuma ya pazia, yani Waafrika wanapewa tuzo saa nne asubuhi wakati kina Beyonce wanapewa jioni.
Yani yupo radhii awe anafanya shows tu kwa ajili ya mashabiki wake lakini sio kwenda kwenye tuzo za BET, huku akisisitiza kuwa anawapenda sana BET
na anatambua mchango wao wa kuwainua wasanii wa kiafrika duniani na
anajua sio rahisi kuandaa tukio kama hilo kila mwaka ila kwa style hii
yupo radhii aende tu kama mtu mwengine wa kawaida kushuhudia tuzo.
Amesema ‘huwa sipost kuhusu kuchaguliwa kuwania tuzo na huwa siongelei pia kwasababu kiukweli sijali’









ULIIONA HII YA VANESSA MDEE AKIZUNGUMZIA ZA MTV 2015? ITAZAME HAPA CHINI….
No comments:
Post a Comment