Monday, June 29, 2015

MO ASSURANCE YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATANZANIA MAONYESHO YA SABASABA‏

IMG_5136
Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama ( wa pili kushoto) akiwa na timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watakaokua wanatoa huduma katika Banda la MO ASSURANCE lilipo ndani ya mabanda ya MeTL Group kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa wa kampuni ya MO ASSURANCE, Mariot Ndomba, Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack pamoja na Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MO ASSURANCE, Esther Moringi.
MO Assurance kampuni ya bima inayohudumia nchi nzima kwa kutoa huduma mbalimbali za bima za majanga ikiwemo ajali ya moto, bima ya wizi, bima za ajali mbalimbali.
“MO Assurance tunapatikana ndani ya jengo la CRDB gorofa ya nane, mtaa wa Azikiwe ambapo tunatoa huduma mbalimbali za bima.” alibainisha meneja masoko msaidizi, Esther Moringi.

Aidha, kwa sasa MO Assurance yenye kauli mbiu ya ‘Amani zaidi, Uhakika zaidi’ ina matawi sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Singida, Arusha na kwingineko. Pia kwa sasa ni miongoni mwa makampuni ya bima nchini yaliyofanikiwa ikiwemo kutoa huduma kwa wateja wa aina tofauti wakiwemo wa ndani na nje wanaoishi nchini.
Kampuni ya MO Assurance ni kampuni Mama ya MeTL Group ambapo unaweza kuwasiliana nao kupitia barua pepe: infomoa@moassurance.co.tz ama kutembelea mtandao wao kupitia : moassurance.co.tz
IMG_5122
Kutoka kushoto ni Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama, Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya mo ASSURANCE, Esther Moringi, Afisa wa MO ASSURANCE, Mariot Ndomba pamoja na Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack katika picha ya pamoja wakiwa tayari kutoa huduma kwa wateja mbalimbali watakaotembelea katika Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
IMG_5118
Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack akipiga 'selfie' na wafanyakazi wenzake.
IMG_5210
Ofisa Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack katika picha ya pamoja na mbunifu wa mavazi nchini, Ally Rehmtulah alipotembelea banda la MO ASSURANCE.
IMG_5234
Muonekano wa nje wa banda la kampuni ya MO ASSURANCE ndani ya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa yalioanza kurindima katika viwanja vya Sabasaba katika barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...