Saturday, May 16, 2015

BARNABA, PIPI NA RUBY WATINGA GLOBAL TV ONLINE

Barnaba akimpigia gitaa pipi aliyekuwa akiimba wimbo wake mpya wa Shauri Yako.
Pipi akijibu moja ya swali aliloulizwa na waandishi (hawapo pichani).
Barnaba akifanyiwa mahojiano na Shorvieny Mohamed katika kipindi cha Mtu Kati.
Pipi akiwa katika pozi.

Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake.
Msanii chipukizi anayekuja kwa kasi, Ruby akiimba wimbo wake wa Na Yule.
Ruby akiwa katika pozi baada ya mahojiano na Global TV.
Ruby baada ya mahojiano.
MASTAA wa muziki wa Bongo Fleva, Pipi Doreen, Barnaba pamoja na chipukizi anayekuja kwa kasi kunako Jumba la Kuibua Vipaji (THT), Ruby jana wametinga kwa mara ya kwanza ndani ya mjengo wa Global Publishers uliopo Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Pipi aliyewahi kubamba na ngoma ya Njia Panda miaka minne iliyopita akiwa na Barnaba aliongelea mengi kuhusiana na ukimya wake kimuziki na kuwa kilichomfanya kuwa kimya kwa kipindi ni kuwa alikuwa ameolewa na kulea watoto wawili.
“Nimerudi upya na ujio wa safari hii ni zaidi ya ule wa njia panda ambapo nimekuja kivingine na wimbo mpya ujulikanao kama Shauri Yako nilioutengeneza chini ya studio ya Barnaba,” alisema Pipi na kuongeza kuwa ngoma hiyo anaiachia leo kuanzia saa kumi na moja.
Naye mkali wa R&B aliyeshtua vichwa vya mastaa wa Bongo Fleva, Ruby aliongea mengi kuhusiana na kutoka kwake kimuziki na safari nzima.
“Walioko juu niwaambie tu nakuja huko. Nimeshatengeneza video ya wimbo wa Na Yule na natarajiwa kuiachia leo jioni katika TV mbalimbali Bongo,” alisema Ruby.
(Stori: Andrew Carlos/GPL)

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...