Saturday, May 16, 2015

DIAMOND AMUITA JOKATE MAKOMBO

DONGO! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemuita mpenzi wake wa zamani Jokate Mwegelo kuwa ni makombo na kudai kama zilipendwa huyo anatembea na hasimu wake Ali Kiba, hakuna jipya kwani anakula makombo.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Diamond ametoa kauli hiyo Jumatano iliyopita wakati mwanahabari wetu alipotaka kujua anajisikiaje kuona wapenzi wake wa zamani Jokate na Wema Sepetu ‘Madam’ wanamuunga mkono Ali Kiba.
Pamoja na kudaiwa kuwa Jokate ana uhusiano wa ‘kimalovee’ na Ali Kiba na mwenyewe kutokubali, ameungana na Wema kuendesha kampeni ya nguvu kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu wampigie kura Kiba kwenye Tuzo za Kili 2015 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya kuuangusha ufalme wa Diamond kimuziki.
Baada ya mwanahabari wetu kuujua ‘mchezo huo’ uliopamba moto kama moto wa kifuu mitandaoni ndipo alipomuuliza Diamond anauzungumziaje ambapo kwanza alikiri kuufahamu na kudai ameudharau maana hauna jipya.
Jokate Mwegelo.
“Hamna jipya waache waendelee kumpigia kampeni (Kiba) lakini mimi nafanya muziki wangu, mashabiki wanafahamu. Kwa hao watoto wa kike, hakuna kipya kwangu si kimuziki hata maisha yao binafsi.
“Wema namjua vizuri, Jokate ndiyo usiseme. Mwache huyo Kiba aendelee kula makombo kwa Jokate kama ameamua kipita njia nilizopita si mbaya, inaruhusiwa,” alisema Diamond.
Jitihada za kumpata Jokate ili aweze kufunguka kuwa anajisikiaje kuitwa makombo na Diamond hazikuzaa matuda kufuatia simu yake kuita bila kupokewa, jitihada zinaendelea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...