Thursday, April 16, 2015

SERIKALI YAMRUDISHA MADENI KIPANDE IDARA KUU YA UTUMISHI KUPANGIWA KAZI NYINGINE

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Ndugu Madeni Kipande.
Itakumbukwa mnamo tarehe 16 Februari, 2015 Waziri wa Uchukuzi Mh.Samuel Sitta (Mb.),alimsimamisha kazi kwa muda Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Ndugu Madeni Kipande ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma mbalimbali dhidi yake.
Tume aliyoiteua Mheshimiwa Waziri kuchunguza suala hili,ilikamilisha kazi yake mnamo tarehe 20 Machi ,2015 na kumkabidhi taarifa ya uchunguzi wao mnamo tarehe 24 Machi 2015 kwa hatua zaidi .
Baada ya kuisoma taarifa ya Tume na hatimaye kushauriana na taasisi mbalimbali zinazohusika na Masuala haya ,tumeridhika pasipo Mashaka yoyote kwamba isingefaa Ndgu Madeni Kipande kuendelea na kazi ya Kuongoza Mamlaka ya Bandari. Hii ni kutokana na kudhihirika utawala mbovu aliouendesha ambao uliosababisha manung'uniko mengi miongoni mwa wateja na wadau wa Bandari na mgawanyiko mkubwa wa Wafanyakazi.
Kutokana na hali hiyo ,Serikali imeamua kumrejesha Ndgu Madeni Kipande idara kuu ya Utumishi ili aweze kupangiwa majukumu mengine.
Ndugu Awadh Massawe ataendelea kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari.
Imetolewa na Wizara ya Uchukuzi
16 April, 2015

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...