Joseph Ngilisho, Arusha
Aibu! Peace Sylvester
(36), mkazi wa Kijenge Juu jijini hapa amefungua madai mazito kwenye
Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha kwa majadala mawili, AR/RB/4404/2015
KUTISHIA KUUA KWA MANENO na AR/RB/5290/2015 KUTELEKEZA FAMILIA dhidi ya
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda jijini hapa katikati ya wiki
iliyopita, Peace alidai Askofu Bagonza ni mzazi mwenzake kwa kuzaa naye
watoto wawili, Piana Bagonza (6) na Bariki Bagonza (3) lakini akadai
amemtelekeza hivyo kuwa na maisha magumu katika kuwalea watoto hao.
AANIKA HISTORIA NDEFU
Peace alisema alianza kufahamiana na askofu
huyo mwaka 2006 mjini Karagwe, Kagera akiwa ni muumini wa kanisa hilo
akimtumikia Mungu kwa kuimba kwaya ya kanisa.
Alisema katika kuonana mara kwa mara na askofu huyo ndipo uhusiano ukaanza lakini kwa makubaliano ya kutunza siri.
“Askofu aliniambia ana mke lakini ananipenda na anataka kuwa na
uhusiano na mimi. Aliniahidi kunisaidia masuala mbalimbali iwapo
nitamkubalia.“Baada ya muda niliamua kumkubalia, tukawa na uhusiano na
tulikuwa tunakutana mara kwa mara. Ilipofika mwaka 2008 nikapata
ujauzito wa mtoto wa kwanza,” alisema Peace.
AHAMIA ILEMELA, MWANZA
Mwanamke huyo aliendelea kudai kuwa, baada
ya kupata ujauzito, askofu huyo aliamua kumhamishia Ilemela mkoani
Mwanza na kumpangishia chumba ambapo mwaka 2009 alijifungua mtoto wa
kike, Piana.
AHAMIA ARUSHA
Peace aliendelea kudai: “Mtoto wangu alipofikisha
umri wa miaka miwili, yaani mwaka 2010, askofu alinihamishia hapa
Arusha na kunipangia chumba eneo la Kijenge Juu na kunitafutia kazi
kwenye Hoteli ya Safari (New Safari Hotel). Hii hoteli inamilikiwa na
KKKT.” Alisema: “Askofu alikuwa akija hapa Kijenge kumsalimia mtoto na
kumwachia matumizi mbalimbali huku akisisitiza kutunza siri zaidi.”
ANASA MIMBA YA PILI
“Ilipofika mwaka 2011 nilipata ujauzito
mwingine wa askofu ila cha kushangaza nilipomfahamisha aliniambia hataki
kusikia taarifa hizo.“Niliweka msimamo wa kutotoa ujauzito na yeye
akasitisha huduma mbalimbali ikiwemo fedha za malipo ya chumba
alichonipangia.
“Alianza kunipigia simu na kunitisha kuniachisha kazi aliyonitafutia
hotelini bila kupewa malipo yoyote. Alikuwa akinitumia watu mbalimbali
kunitishia maisha. “Kutoka na hali hiyo nililazimika kumtafuta kiongozi
mmoja wa ngazi ya juu kanisani na kumwambia jinsi askofu
alivyonitelekeza kwa zaidi ya miaka minne bila kunihudumia nikiwa na
watoto wake wawili.
“Hata hivyo, kiongozi huyo aliniambia atalishughulikia suala langu,
lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na nikimkumbusha amekuwa
akinijibu kwa ukali na kunikatia simu.”
WATOTO HAWAENDI SHULE
Peace alisema: “Kwa sasa naishi kwa shida na watoto. Hawaendi shule baada ya kukosa ada.”
ASKOFU NA IJUMAA WIKIENDA
Akizungumza kwa simu na gazeti hili
huku akihifadhiwa sauti, Askofu Bagonza alikiri kumtambua Peace kama
mzazi mwenzake ila alisema si kweli kama hamtumii matumizi.“Mbona fedha
huwa namtumia labda ameamua kunichafua tu. Hata juzi nimemtumia shilingi
250,000 iweje asema simhudumii?” alisema askofu huyo na kukata simu.
Kwa upande wake, Peace alipoulizwa kuhusu kutumiwa kiasi hicho cha
fedha, alisema: “Fedha hizo nilizipokea kutoka kwa wakala wa M-Pesa
baada ya jambo hilo kulifikisha kwenye vyombo vya dola (polisi).”Taarifa
zilizolifikia gazeti hili wakati linakwenda mitamboni zilieleza kuwa
mwanamke huyo ameitwa Karagwe kwenda kuongelea suala hilo.
No comments:
Post a Comment