Sunday, April 19, 2015

SIWEMA, SHAMSA PACHIMBIKA


Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ , Siwema.
Imelda mtema
Kazi imeanza! Staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford ambaye kwa hivi sasa ni mpenzi mpya wa mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wa zamani wa Mbongo-Fleva huyo, Siwema wameanza kuchimbana baada ya hivi karibuni kurushiana madongo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shamsa aliposti picha na maneno akielezea kuwa anajiona ni mwanamke bora kwa kuwa ameweza kuzaa kwa njia ya kawaida na Mungu amemuepusha na kujifungua kwa kisu ambapo posti hiyo ilimkera Siwema.
Staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford.
Kwa upande wake Siwema, aliichukua posti hiyo kama ilivyo na kuibandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alianza kumchamba Shamsa kuwa siyo kwamba alipenda kuzaa kwa oparesheni ila alishauriwa na madaktari hivyo asijione amefika kwa Nay maana akitaka kurudi hatatumia hata sekunde. Mwandishi wetu aliwatafuta wawili hao ili kujua kulikoni ambapo Siwema alisema kuwa amechoshwa. Kwa upande wake Shamsa alisema hataki kuzungumza chochote atampa ‘kiki’.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...