Sunday, March 1, 2015

WAJUE PLATINUM, WAPINZANI WA YANGA MICHUANO YA SHIRIKISHO

FC Plutinum
Yanga SC
Yanga imeendelea kubaki katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, ambapo baada ya kuruka fitna za Waswana, sasa wamehamia kwa Robert Mugabe, baada ya kupangiwa kukutana na FC Plutinum ya Zimbambwe, ambayo iliwang’oa Sofapaka ya Kenya katika mchezo wa mkondo wa awali uliopigwa jana Jumamosi.
Yanga imechupa katika hatua ya kwanza kufuatia kufunza adabu BDF XI ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2, huku Plutinum wao wakipenya kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia juzi kushinda tena kwa mabao 2-1.
Kwa mujibu wa duru za spoti, wapinzani wa Yanga wanaonekana kuwa wakali wakiwa na makombe kadhaa kwenye ligi ya kwao.
Platinum ilianzishwa mwaka 1995 na mwaka jana ilimaliza katika nafasi ya 4 katika ligi kuu nchini kwao na kunyakua takribani makombe 4.
Makombe waliyochukua ni pamoja na;
Chibuku Super Cup  
Independence Cup 
 ZNA Charity Tournament 2014
na CG Msipa Charity Tournament 
2014.
Yanga wataanza mchezo wao ugenini, mchezo utaopigwa katika uwanja wa Mandava (Mandava stadium) kisha kurudiana nao hapa nyumbani katika dimba la Taifa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...