Tuesday, March 17, 2015

KAKA WA JOSE CHAMELEONE AK47 AFARIKI DUNIA

Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47 enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI wa dancehall nchini Uganda, Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni.
Wimbo mpya wa marehemu AK47.
Taarifa zimeeleza kuwa kabla ya mauti kumkuta, AK47 alikuwa katika baa moja ya usiku iliyopo eneo la Kabalagala pamoja na marafiki zake.
Imeelezwa kuwa alidondoka akiwa bafuni wakati akiongea na simu na kukimbizwa katika Hospitali ya Nsambya iliyopo jijini Kampala, Uganda ambapo mauti yalimfika.
Chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika japo baadhi ya watu wameeleza kuwa marehemu alivuja damu kwa ndani baada ya kuanguka bafuni.
AK47.
AK47 ni kaka wa wasanii watatu wa nchini Uganda, Jose Chameleone, Weasel na Pallaso na alilelewa katika familia ya wanamuziki ya Gerald Mayanja na Prossy Musoke.
Baada ya taarifa hizo za msiba, kaka zake marehemu walionyesha simanzi zao kwa mashabiki kupitia akaunti zao za Facebook.
Pallaso
Baba wa mbinguni, moyo wangu umesambaratika... Dunia yangu imevunjika!! Nimempoteza rafiki yangu kipenzi, kaka yangu, mtu ambaye anajua kila kitu kuhusu mimi na mimi ninajua kila kitu kuhusu yeye.. Wote tumeleana... Dunia imempoteza mmoja wa malaika wakubwa kuwahi kutokea... Kaka yangu Emmanuel Mayanja aliyezoeleka kwa wengi kama AK47 hatunaye tena!! Mwenyezi Mungu niamshe tafadhali maumivu ni makali mno!!
Marehemu AK47.
Jose Chameleone
Taarifa za msiba!!
Kifo kimetuchukulia mpendwa wetu Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47. Kwa marafiki wetu wote, tunamwomba Mwenyezi Mungu atutue nguvu kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu. Kaka yangu umeondoka mapema mno.
Weasel
RIP bro…..umeondoka mapema mno!
Kupitia mtandao wa Twitter, mwanamuziki Bebe Cool naye aliandika hivi: "Hii ni taarifa mbaya kuwahi kutokea. Nimeambiwa na Meneja wa Leon Island kuwa mdogo wetu AK47 amepoteza maisha"
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU EMMANUEL MAYANJA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!!

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...