Tuesday, March 17, 2015

YEMI ATANGAZA SIKU YA KUZIKWA BABA YAKE


Baba yake Yemi Alade aliyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI wa kike wa Nigeria, Yemi Alade,  na familia yake watafanya  maziko ya marehemu baba yake tarehe 7 na 8 Mei mwaka huu.
Baba yake Alade aliuyekuwa Kamishna Mstaafu wa Polisi, J.A. Alade, alifariki  Januari 16 mwaka huu na binti yake huyo ambaye ni mtunzi wa wimbo maarufu wa ‘Johnny’, hajasema mengi kuhusiana na kifo hicho tangu kitokee.
Mwanamziki wa kike wa Nigeria anayetamba kwa wimbo wa Jonny, Yemi Aladeakiwa katika pozi.
Ni katika mahojiano ya gazeti la Tribune yaliyofanyika Machi 13, mwaka huu (siku ya kuzaliwa kwake) ndipo  aliposema maziko ya baba yake yatafanyika Mei 7 na 8.
Yemi Alade ni mtoto wa mwisho kwa baba yake huyo kutoka kabila la Wayoruba na mama kutoka kabila la Waigbo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...