Thursday, March 19, 2015

EU WAMPA TUZO MAMA HELEN KIJO BISIMBA‏

Dk. Helen Kijo Bisimba akiwa ameshikilia tuzo yake.
Tuzo hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka  wa Maendeleo Ulaya  2015.
Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo  kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.
Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki
Keisha Saban,  Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na  mchoraji.
EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.
Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...