Monday, March 2, 2015

AZAM YAWATIMUA MAKOCHA WAWILI, TIMU APEWA MGANDA

Omog kushoto akiwa na msaidizi wake, Shikanda ambao wote wametimuliwa kwenye viyoyozi vya Complex mchana huu.
  Uogozi wa Azam umetangaza rasmi kuachana na kocha wake, Mcameroon, Joseph Omog pamoja na msaidizi wake, Ibrahim Shikanda kwa kilichotajwa ni kutokana na mbinu za kocha huyo kuonekana kufikia ukingoni.
Omog aliichukua Azam Desemba mwaka juzi, akichukua mikoba ya Muingereza, Stewart Hall ambaye aliachana nao baada ya kupata dili la maana katika Kampuni ya Symbion.

Omog aliiwezesha Azam kutwaa ubingwa wa ligi ku,ukiwa ni wa kwanza kwa klabu hiyo iliyopanda ligi kuu mwaka 2008.

Hata hivyo msimu huu pamoja na kuwa nafasi ya pili, lakini timu hiyo imekuwa na mwendo wa kusuasua, kabla ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-2.

Taarifa ilitolewa na uongozi wa Azam katika Ukurasa wa Facebook, imesomeka;
“Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu, Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
“Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidizi wake Ibrahim Shikanda. Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe.” 
 Kwa upande wa Shikanda alipotafutwa simu yake iliita bila kupokelewa licha ya kupigiwa mara kadhaa.

SABABU ZENYE KUTUPIWA JICHO

Katika sababu ambazo amekuwa akizitaja katika kila mchezo ni safu ya ushambualiji kutokuwa makini, kucheza kwa kutoelewana, sababu ambayo amekuwa akiitoa takribani kila mchezo. Lakini Azam inabaki kuwa timu yenye mafowadi wa viwango vya juu, lakini pia Omog akiwa kwenye kitengo kwa kuwachisha ajira mafowadi.
Azam ina jumla ya mafowadi sita, huku ikiwa chini ya Omog ikiwachinjia baharini mafowadi watatu:
Ismail Kone, Leonel Saint-Preux na Brian Umony ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Saint George ya Ethiopia.
KIWANGO
Ipo wazi kuwa Azam inaamini kuwa timu yenye wachezaji wa viwango vya juu, ina uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote imtakaye kwa jeuri ya hela, lakini chini ya Omog imekuwa ikicheza soka la kueleweka si zaidi ya dakika 60. Ina kila miundo mbinu ya 'fitness' lakini tatizo la pumzi limekuwa sugu kwenye utawala wa Omog.

BEST NSIMBE
Besst Nsimbe kushoto pamoja na C.E.O wa Azam Saad Kawemba.
Kibarua chake cha kwanza kitakuwa Jumamosi, wakati Azam ikiikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanjawa Chamazi, Complex.
Nsimbe, ambaye ni kocha wa zamani wa Kampala City Council Authority ya Uganda (KCCA), amekua na mafanikio makubwa akiipa ubingwa mara mbili, huku pia akiwa na kumbukumbu ya kuwafunga Al Merrik, ambayo iliowatoa juzi.  

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...