Saturday, February 7, 2015

SIMBA, AZAM ZAWEKWA PABAYA VPL WIKIENDI YA SARE !!!!!

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Azam pamoja na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Kagame, Simba zimelazimishwa sare hivyo kujiweka pabaya katika mbio za kuwania ubingwa ambapo wameishusha Yanga presha ya kujikita kileleni.
 
Kiungo wa Simba, Abdi Banda katikati akiwatoka wachezaji wa Coastal Union. Kushoto ni kiungo wa zamani wa Simba, Abdulhalim Humud.


Azam imelazimishwa mabao 2-2 na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri, ambapo mabao ya Azam yakifungwa na mapacha, Kipre Tchetche na Kipre Balou. Mabao ya Polisi yemefungwa na Said Bahanuzi na Kassim Selembe.
Matokeo hayo ni kwamba Azam anafikisha pointi 22, sawa na Yanga lakini wao watashuka dimbani kesho kumenyana na Mtibwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Simba imeendelea kuandamwa na matokeo ya sare, baada ya kulazimishwa suluhu na Wagosi wa Kaya, huku Simba wakipoteza nafasi kadhaa kupitia kwa Elias Maguri, Danny Sserunkuma.
Matokeo hayo yameibakiza Simba na pointi 17, moja nyuma ya Coastal.
Danny Ssernkuma wa Simba (kulia) katika harakati za kusaka bao mbele ya beki na kipa wa Coastal.

Katika kile kilichoonekana wikiendi hii ni mwendo wa sare, napo kwenye Uwanja wa Chamazi, Maafande wa JKT Ruvu walibanwa mbavu na Mbeya City kwa kutoka sare ya bao 1-1. Wafungaji wakiwa ni Ally Bilal kwa upande wa JKT huku Kenny Ally akiifungia City.
Nagwanda Sijaona, wenyeji Ndanda wamebanwa mbavu na Stand kwa kutoshana nguvu ya bao 1-1 huku matokeo kama hayo pia yakipatikana kwa Prisons na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...