Friday, February 6, 2015

SOMA KUMBUKUMBU MUHIMU RAUNDI YA PILI, VPL 2015


Coastal Union  vs Simba

1.   Timu zote zitakuwa na makocha wapya, tofauti na raundi ya kwanza. Simba ipo chini ya Mserbia, Goran Kopunovic badala ya Mzambia, Patrick Phiri. Coastal iko chini ya Mkenya, James Nandwa na sio  Mkenya, Yusuph Chippo.
2.   Amisi Tambwe aliifungia Simba moja ya mabao katika sare ya mabao 2-2, lakini sasa si mali tena ya Simba, yupo mtaa wa pili pale Jangwani.
Tambweee..... akiifungia Simba lakini kesho haitakuwa nao 

3.   Haruna Chanongo alikuwa mwiba mkali siku hiyo kwa ngome ya Coastal lakini safari hii yuko zake Stand United.
Chanongo kushoto akikwepa daruga la mchezaji wa Coastal 

4.   Abdulhalim Humud kwa mara ya kwanza anakutana na timu yake ya zamani ya Simba, baada ya kujiunga na Coastal Union, akitokea Sofapaka ya Kenya katika dirisha dogo la usajili.

Yanga vs Mtibwa
1.   Yanga inaingia na benchi nzima jipya. Katika mchezo wa kwanza, ilikuwa na jopo la makocha watano- Wabrazili, Marcio Maximo na Leonardo Neiva wakisaidiana na wazawa, Shadrack Nsajigwa na Salvatory Edward na kichapo juu, lakini safari hii iko chini ya Mdachi, Hans van Der Pluijm akisaidiana na Mzawa, Charles Mkwasa.

Benchi la Yanga katika mchezo wa raundi ya kwanza. Maximo (mwenye kitabu), kutoka kulia ni aliyekuwa msaidizi wake Neiva, Edward kushoto kwa Maximo na Nsajigwa.

Benchi jipya la Yanga, kutoka kushoto ni Pluijm, Mkwasa, Juma Pondamali (kocha wa makipa)

2.   Geilson Santana ‘Jaja’ ambaye anabaki kuwa staa wa Ngao ya Hisani, hayupo pamoja na Mganda, Hamisi Kiiza ambao walifurukuta katika mchezo wa kwanza hawapo leo hii.
Jaja wa 'Ngao ya Hisani' mwenye jezi namba 9 hayupo Yanga tena.

3.   Mtibwa inakutana na Yanga iliyojaa sura mpya katika safu ya ushambuliaji, Kpah Sherman, Tambwe, Danny Mrwanda ambao mchezo wa awali hawakuwepo.
4.   Mbrazili, Andrey Coutinho iwapo atacheza mchezo wa kesho, itakuwa ni rekodi kwake kwani katika mchezo wa kwanza alikuwa anaumwa.
Azam  vs Polisi Moro
1.   Ni ngumu kumuona Aggrey Moriss katika mchezo wa kesho na mechi mbili nyingine za Azam kutokana na kutumikia kifungo cha mechi tatu alichokumbana nacho kutoka kwa TFF, mapema leo hii.
2.   Mrwanda aliwatesa sana mabeki wa Azam na kufunga bao pekee katika kichapo cha mabao 3-1 pale Chamazi, lakini leo hii nguvu za Polisi zipo kwa Said Bahanuzi aliyetokea Yanga.
Mrwanda, mwenye jezi namba 7 si mali ya Polisi tena, yupo Yanga. Pia Moriss wa Azam (wa kwanza kushoto) haiwezekani kucheza mchezo wa wikiendi hii.

3.   Kaptaini, John Bocco ana uhakika wa kucheza mchezo huo, tofauti na raundi ya kwanza ambapo timu yake ya Azam ilikosa huduma yake.
The Captaaaaniiiiii....John Bocco kesho ndani ya dimba.

4.   Kali Ongalla hayupo katika benchi la Azam badala yake kuna Mganda, George Best Nsimbe ambaye ndiye msaidizi wa Mcameroon, Joseph Omog.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...