Saturday, February 7, 2015

GIOVINCO; JAMAA ANA NYOTA YA KUWANGA


Sijui kosa langu...Fowadi wa zamani wa Juve, Giovinco ameamua kuikimbia nchi ya Italia, baada ya kuchoshwa na maisha ya kipweke! Hapendwi

 Straika wa Kiitalia, ambaye amejiunga na klabu ya Toronto ya huko Canada, Sebastian Giovinco ametoa kali ya mwaka baada ya kuweka bayana kuwa aliamua kuondoka nchini kwao, kutokana na kutopendwa  na wengi.
Nyota huyo, 28, aliyejiunga na Toronto akitokea Juventus ameonekana kuwa alikuwa hana mahusiano mazuri na kila mtu, kuanzia vyombo vya habari hadi makocha waliopata kuifundisha Juve, akiwemo Antonio Conte, Massimiliano Allegri  na Cesare Prandelli.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika vyombo vya habari, muda mfupi baada ya kutua Canada, tayari kuungana na timu yake mpya,   Giovinco alifunguka kuwa alilazimika kuondoka Juve baada ya kuchoshwa na kujiuliza juu ya uwezo wake wa sasa.
"Pale Italia nilikuwa na matatizo mengi sana. Kila siku hakuna kingine cha kusema zaidi ya kujadili kiwango changu kwamba siwezi kucheza katika kiwango cha juu, lakini nilikuwa nikipinga katika hilo kila siku tena kwa hoja," alisema Giovinco.
"Nilitamani nitafute mji ama timu ambayo ingenikaribisha vizuri, kama hii ilivyonipokea. Kwa hiyo ujio wangu huku ulikuwa sahihi."
Lakini pamoja na hoja yake na shutuma kwa maelewano mabaya na makocha wake pamoja na media kwa kulia kuwa hakupewa muda wa kucheza, lakini takwimu zinakinzana na maneno yake kwani.
Katika msimu wa 2012/13 nyota huyo alipewa nafasi mara 31 kwenye ligi kuu na kufunga mabao saba tu  wakati kikosi chake kikitwaa ubingwa wa ligi hiyo maarufu kama Serie A, ikiwa ni mara ya tatu mfululizo.
Msimu uliopita 2013/14 alicheza mechi 17 za Serie A, zikiwemo sita akianza na akafunga mabao mawili tu, huku msimu huu amezidi ‘kuharibu’ kwani amecheza mechi saba  na kuanza mechi mbili na hajafunga bao lolote.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...