Timu ya DR Congo imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika
michuano ya Kombe la Mataifa Afrika Afcon 2015, baada ya kuwaondoa wenyeji,
Guinea ya Ikweta katika changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2, baada ya mchezo
huo kumalizika suluhu.
Michuano hiyo itahitimishwa rasmi kesho wakati Ivory Coast
itakapomenyana na Ghana katika Dimba la Bata nchini Guinea ya Ikweta, ambapo
michuano hiyo imeandaliwa.
Wakali wa bolingo wamejipatia nafasi hiyo baada ya kufanya
kweli katika mikwaju ya penalti ambapo walipata yote na wapinzani wao
wakiambulia miwili, huku mlinda mlango na nahodha Robert Kidiaba akiokoa mkwaju
mmoja kati ya hiyo.
Mikwaju ya DR Congo ilifungwa na Cedrick Mabwati, Lema Mabidi, Chancel
Mbemba na Gabriel Zakuani, wakati wa wenyeji Guinea Ikweta yaliwekwa kiamiani
na Ellong Doulla na Juvenal Owono, huku Raul Bosio mkwaju wake ukimezwa na
Kidiaba, wakati Javier Balboa uliota mbawa.
The Hero.... Kidiaba alipangua moja ya mikwaju ya Guinea Ikweta. |
Hata hivyo, katika mchezo huo Guinea Ikweta walionekana
kutokuwa na hamasa, ikiwa ni siku chache
tangu mashabiki wao wafanya vurugu uwanjani baada ya kichapo takatifu
cha mabao 3-1 walichopokea kutoka kwa Ghana katika mchezo wa nusu fainali.
Wakati Ivory Coast, wao walitinga fainali baada ya kuwavuruga DR Congo kwa
mabao 3-0.
Uzalendo haswa...mashabiki wa DR Congo |
No comments:
Post a Comment