Monday, February 2, 2015

MSAIDIZI WA PHIRI AIWEKA KIPORO NAFASI YA MATOLA SIMBA

 
Jap Staam wa tatu kutoka kushoto akiwa na Patrick Phiri wa kwanza kushoto, enzi wakiwa wote Simba msimu 2010/11
Beki na kocha wa zamani wa Simba, Amri Said ‘Jap Staam’ amesema anatamani kurejea klabnuni hapo kuchukua mikoba ya Seleman Matola aliyeomba kujiweka pembeni, lakini kikwazo pekee ni mkataba mrefu na Mwadui.
Staam ni kocha msaidizi wa Mwadui akifanya kazi na jmahuri Kihwelo ‘Julio’.
Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi enzi za Patrick Phiri msimu wa 2010/11, alisema mkataba huo na Mwadui unamnyima nafasi ya kurejea klabuni kwake na kuongeza kuwa akili yake kwa sasa ni kuisaidia Mwadui kuhakikisha inapanda ligi kuu msimu 2015/16.
“Ni kweli Simba ni timu yangu, naipenda lakini kwa sasa siwezi kusema chochote kutokana na mkataba wangu na Mwadui kunibana. Najua ni nafasi nzuri kwa kocha yeyote mwenye mapenzi na timu, lakini kwa sasa akili yote tumeilekeza katika mechi mbili zilizobaki dhidi ya Polisi Tabora na Burkina Faso ambazo iwapo tutashinda tunapanda ligi kuu,” alisema Staam.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Matola alitangaza kuachia ngazi ya ukocha msaidizi, ambayo haijapata mtu mpaka sasa.
Jap Staam katikati, akiwa na benchi la ufundi la Mwadui ya Shinyangam inayoshiriki ligi daraja la kwanza. Wa kwanza kulia ni kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio'

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...