Monday, February 2, 2015

PLUIJM: WACHEZAJI WANGU HAWAJIELEWI

Kocha Mkuu wa Yanga, Pluijm (wa kwanza kulia), haamini kile wachezaji wanachofanya siku ya mechi

Kitendo cha timu ya Yanga kuendelea kupata matokeo ambayo si mazuri kulinganisha na matarajio ya wengi, kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema kuwa hajui tatizo liko wapi kwani kila mbinu anawafundisha na wanafanya vema mazoezini lakini siku ya mechi wanacheza ndivyo sivyo.
Tofauti na matarajio ya wengi ya kushuhudia mvua ya mabao kutokana na uwepo wake akiwa na rekodi nzuri ya msimu uliopita ambacho kiliandikisha rekodi ya ushindi mkubwa wa mabao 7-0 katika mechi mbili huku kikifunga mabao 19 katika mechi tatu mfululizo; dhidi ya Komorozine, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons, lakini mambo si mambo kwani msimu huu timu hiyo haijashinda zaidi ya mabao mawili.
Katika mechi tatu zilizopita, Yanga imepata bao moja; dhidi ya Polisi Moro huku ikishikwa shati uwanja wa taifa mbele ya Ruvu Shooting na Ndanda.
Akizungumzia kikosi chake, Pluijm alisema, “Hata sielewi kabisa tatizo la kikosi changu liko wapi, ninawapa kila mbinu lakini wawapo kwenye mechi sijui nini kinatokea, lakini nadhani tatizo hili linatakiwa lkufanyiwa kazi zaidi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa msimu huu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...