Thursday, February 5, 2015

MREMA AMSHITAKI BUNGENI MH.MBATIA KWA KUMTANGAZIA KUWA ANA UGONJWA WA UKIMWI

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Augustine Mrema (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, ndani ya jengo la Bunge.

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya  chama cha TLP, Augustine Mrema, leo muda mfupi kabla ya shughuli za Bunge kukamilika Mwenyekiti wa Bunge hilo Mh. Mussa Hassani Zungu, ameweza kumpatia nafasi na kutoa hoja yake binafisi iliyokuwa ikilenga kumtuhumu Mbunge wa kuteuliwa Mh.Mbatia kwa kumtangazia kwa Wananchi wa jimbo lake kuwa ana ugonjwa wa Ukimwi na kwamba wasichague wenye viti wa Chama hicho maana Mrema hataweza kugombea uchaguzi ujao kutokana na afya yake kuasiliwa na maradhi hayo.
Mrema alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa Mbatia amewatangazi pia wananchi wake kwamba amedhamilia kukiua chama hicho na kwamba kila kinachohusiana na chama cha TLP wampatie yeye ili uchanguzi ujao aweze kuwafanyia mengi zaidi.POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...