Thursday, February 5, 2015

INGIA HUMU UONE JINSI RAIS WA ZIMBAMBWE ROBERT MUGABE ALIVYO PIGA MWELEKARais wa Zimbambwe Robert Mugabe akiwa ameanguka muda mfupi baada ya kukosea ngazi alipokuwa akishuka tayari kwa kuingia kwenye gari lake kwenye Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo alipokuwa akitokea nchini Ethiopia.
HATIMAYE picha zinazoonyesha tukio la kudondoka kwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 90, zimezidi kusambaa kwa kasi huku baadhi ya watu wanaojua kucheza na teknolojia wakizibadili na kulifanya tukio kama la utani.
Ukweli wa tukio hilo ulikuwa hivi, Mh. Mugabe alidondoka Ijumaa iliyopita katika Uwanja wa Ndege wa Nchi hiyo, muda mfupi tu bada ya kukosea kukanyaga moja ya ngazi ya jukwaa alilokuwa akiongelea, mara baada ya kutua hapo akitokea nchini eiThiopia ambako alienda kwaajili ya shughuli zake za kiserikali.
Mugabe alianguka mpaka chini mara tu baada ya kumaliza kuzungumza na baadhi ya wafuasi wake waliyojitokeza kumpokea kwenye Uwanja wa ndege wa nchi hiyo.

Rais Mugabe akiwa chini baada ya kudondoka.

Picha hizi zimekuwa dili na wengine kuzichezea kama inavyoonekana picha hii.
 

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...