Sunday, February 1, 2015

ANGALIA MATUKIO MBALIMBALI YA SHEREHE YA MIAKA 10 YA THT

 Msanii kutoka katika Nyumba ya kukuzia Vipaji Tanzania 'THT', Barnaba Boy (kulia), akitumbuiza na msanii mchanga wa THT, kwenye sherehe za kutimiza miaka 10 ya Taasisi hiyo zilizofanyika katika Ukumbi wa Escaper One Mikocheni jijini Dar es Salaam Usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa Hip Hop Bongo, Mwana FA (kushoto), wakiimba kwa pamoja na Ali Kiba wimbo wa Kiboko yao waliyoshirikiana kwa pamoja kwenye sherehe za Mika 10 ya THT usiku wa kuamkia leo.
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ( wa tano kutoka kushoto), akicheza na baadhi ya wasanii wa THT, muda mfupi baada ya kukaribishwa jukwaani hapo kwaajili ya kusema machache juu ya sherehe hizo.
 Baadhi ya mashabiki waliohudhuria kushuhudia sherehe hizo wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio yaliyokuwa yakijili ukumini hapo.
 Msanii Barnaba Boy akionyesha umalidadi wake katika kutumia Gitaa.
 Ben Pool akitoa burudani mahali hapo.
 Baadhi ya wasanii wachanga wa THT, wakiimba kwa pamoja.
 Amini akiimba wimbo wake mpya huku akiwa amekumbatiwa na mkewe aliyepanda jukwaani hapo baada ya kuguswa na wimbo huo na kuanza kuangua kilio.
 Mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima (kulia), akishuhudia burudani zilizokuwa zikiendelea ukumbini hapo na Mumewe.
 Baadhi ya wasanii wa THT, wakiwa katika pozi nyuma ya jukwaa lililokuwa likitumika kutolea burudani ukumbini hapo.
Kadja Maumivu akiimba kwa hisia kali katika jukwaa hilo.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...