Sunday, February 1, 2015

OWINO KUREJEA KIKOSINI SIMBA SC


Habari  njema kwa mashabiki wa Simba ni taarifa za kurejea kwa mlinzi wa kati, Mganda, Joseph Owino ambaye anatarajia kurejea kikosini mwezi huu.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Humprey Nyasio amesema nyota huyo wa zamani wa Azam, amekuwa akisumbuliwa na jeraha za nyama za paja, lakini taarifa za kitatibu zinadai atakuwa fiti kuanzia mwezi ujao-Februari.
Safu ya ulinzi ya timu hiyo imeonekana kupwaya hivi karibuni kwa kuruhusu mabao mepesi, hali ambayo
Akizungumza na blogu hii, Nyasio alisema:
“Owino bado hajapona vizuri lakini kwa mujibu wa daktari, tutakuwa naye kuanzia mwezi ujao,” alisema Nyasio.
Safu ya kati ya ulinzi ya timu hiyo kwa sasa inasimamiwa na nahodha Hassan Isihaka na Mganda, Juuko Murshid.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...