Saturday, January 31, 2015

KOCHA SIMBA AILIZA NDANDA, ATAJWA KIKWAZO CHA TIMU


The Hero.... Staam anatajwa kuwa shujaa wa Ndanda ambayo haijafanya vema ligi kuu bara


Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, Amri Said 'Jap Staam' ametajwa kuwa mchawi wa timu ya Ndanda ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu imekuwa na mwendo wa ‘bata’ tofauti na kasi iliyokuwa nayo kwenye ligi daraja la kwanza.

Said maarufu zaidi kwa jina la Staam, kwa sasa yupo na kikosi cha Mwadui akisaidiana na Jamhuri ‘Julio’ Kihwelo ambayo ina nafasui nzuri ya kupanda ligi kuu msimu ujao iwapo tu itashinda mechi zake dhidi ya Polisi Tabora na Burkina Faso.

Habari zilizopatikana zinadai kuwa mashabiki wa timu ya Ndanda wamekuwa wakiuliza kuondolewa kwa kocha huyo, kwani timu ilikuwa ikifanya vema enzi za kipindi chake tofauti na sasa kwenye ligi kuu.

Kwa upande wa Staam alipoulizwa kama anaweza kuwasikiliza tena Ndanda, alisema: “Mhh…ni ngumu ndugu yangu, kwanza nina mkataba na Mwadui na pia kwa kipindi kama hiki ni vigumu maana siwezi kuichukua timu katikati ya msimu, labda ingekuwa mwishoni mwa msimu ili niweze kuanza program zangu mwenyewe,” alisema Staam.
Unakumbukwa sana na Wana Kuchele wa Ndanda

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...