Thursday, January 29, 2015

BAADA YA KUNASA SAINI YA PAULISTA, WENGER AAPA KULA SAHANI MOJA NA KINDA WA VALENCIA

 Anatakiwa Emirates... Kiungo chipukizi wa Valencia, Jose Gaya anahitajika na klabua ya Arsenal kwa vyovyote vile!

Klabu ya Arsenal imeanza mazungumzo na Klabu ya Valencia ya huko Hispania, kutaka saini ya kinda wao Jose Luis Gaya, baada ya kumtengea kitita cha pauni milioni 13.5.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Express tayari Arsenal wameweka hadharani nia  hiyo.
Hata hivyo kinda huyo amekuwa akitolewa macho na vigogo wa hela duaniani, Real Madrid lakini bado haijajulikana kama Arsenal wataendelea moto huo baada ya Madrid kuingilia dili lao mchana leo hii.
Klabu yake ya Valencia haina matarajio ya kumuachia kinda huyo lakini 'mzigo' wa maana ambao wanaweza kutengewa na klabu nyingine hususan za England, zitawashawishi kumuachia kinda huyo.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...