Thursday, January 29, 2015

ARSENAL YAMFUNGIA KAZI SUAREZ, YASEMA NI LAZIMA AREJEE ENGLAND


Alikwenda kutalii Barca?, Suarez anatakiwa na Arsenal.
Timu ya Arsenal imeanza mbio za kuhakikisha inamnasa fowadi wa Barcelona anayepigana kupandisha jina lake, Luis Suarez, Gazeti la The Sun limeripoti.
Suarez, mwenye miaka 28 alijiunga na Barcelona
msimu huu katika majira ya joto, lakini amekumbana na changamoto kubwa huku mashabiki wa timu hiyo wakiamini kuwa hajaonesha kiwango cha maana, ikiwa  amefunga mabao mawili tu kwenye ligi kuu, La Liga.
The Sun limeripoti kuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemfungia kazi, ambapo bado ana kumbukumbu ya kuwahi kumhitaji wakati akiwa Liverpool kwa kumtengea kiasi cha pauni 40,000,001 mwaka 2013, lakini zikakataliwa na  timu yake ya Liverpool.
 

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...