Wednesday, April 2, 2014

GLOBAL YAFANYA MAUAJI, YAICHAPA NSSF 6-1

TIMU ya Global Publishers Ltd leo imetoa dozi ya mabao 6-1 kwa timu ya NSSF katika mechi yao ya ufunguzi wa Michuano ya Kombe la NSSF iliyopigwa Uwanja wa TCC Chang'ombe, Temeke jijini Dar. Mabao ya Global yamewekwa kimiani na Musa Matora, Ally Mbetu, Christian Kimbe na Omar Hamis aliyetupia matatu 'hat trick'. Kwa matokeo hayo, Global wamesonga mbele katika michuano hiyo.

Mshambuliaji wa Global Publishers Ltd, Saleh Ally, akiwatoka mabeki wa timu ya NSSF.


Mtanange kati ya Global na NSSF ukiendelea.


Mshambuliaji wa NSSF akiambaa na mpira. Pembeni ni kiungo wa Global, Musa Matora, akijaribu kumzuia.


Kiungo mkabaji wa Global, Juma Ramadhan, akijiandaa kupiga mpira wa adhabu ndogo.


Patashika langoni mwa Global.


Salaeh Ally akiwania mpira na beki wa NSSF.


Kikosi cha Global wakati wa mapumziko.


Kikosi cha Global kabla ya mechi na NSSF.


NSSF wakiwasalimia wachezaji wa Global.


Timu za Global na NSSF kabla ya mtanange kuanza.


Kikosi cha Global kikipanga mikakati kabla ya mchezo.


Kikosi cha NSSF.


Mshambuliaji wa Global, Omar Hamis, aliyetupia mabao matatu 'hat trick' akikabidhiwa mpira wake na mwamuzi wa mchezo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...