Sunday, March 2, 2014

SEHEMU YA KWANZA YA UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA - MUNGU HABADILIKI UBUNGO PLAZA

Siku ya jana ilikuwa ni siku ya furaha na ndelemo katika ukumbi tulivu wa Ubungo Plaza katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya mwimbaji maarufu Tanzania Mess Jacob Chengula alipokuwa akizindua albamu yake ya "Mungu Habadiliki" Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji zaidi ya 20 waliovamia jukwaa na kuwaacha watu kupagawa na uwepo wa Mungu ulioachiliwa kwa njia ya uimbaji. Viti vilikuwa havikaliki na kuwaacha  ma-MC kuwa katika wakati mgumu sana wa kuwaomba watu wakae chini.

Kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao, mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.

Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.

Mgeni rasmi Januari Makamba alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji. Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika huduma yao ya uimbaji.

Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao. Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.

Picha zimepigwa na RumAfrica
+255 715 851523

Tembelea
www.messchengula.blogspot.com

TUONE BAADHI YA MATUKIO SEHEMU YA KWANZA

Mkurugenzi wa RumAfrica Rulea Sanga (wa pili kutoka kulia) tembelea blogu yake www.rumaafrica.blogspot.com


Rulea Sanga
Viti maalumu kwaajili ya Mgeni rasmi na crew yake.

Wauzaji wa tiketi

Tiketi zilizotumika katika uzinduzi huu. Kazi imefanywa na RumAfrica +255 715 851523



Masanduku yaliyobeba DVD za Mungu Habadiliki kabla ya kuzinduliwa

MC Chiwalo wa Wapo Radio na Boniface Magupa wa PPR

Miriamu Lukindo
Blogger Jimmy akiwa kazini
Ibarahimu Sanga


Betrice Mwaipaja

Bahati Bukuku
Atosha Kissava
Atosha Kissava
 Jerry
Kiza Blessing

Mwinjilisti Sarah Mvungi
MC Boniface Magupa

Joshua Makondeko na madanza







 Atosha Kissava (kulia)


USIKOSE KUANGALI SEHEMU YA PILI







No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...