Monday, March 3, 2014

R. KELLY ALIYEWAHI KUOKOKA SASA APIGA PICHA ZA UCHI KATI YA MPENZI WA CHRISTIANO RONALDO (IRINA SHAYK)


Mungu aweza kumuokoa mtu, Mungu aweza kukupa uhuru wa kumtumikia au kutomtumikia, Mungu anakupa nafasi ya kumtumikia, Mungu hakulaazimishi kumtumikia au kutomtumikia ila ni wewe kuamua. Mungu alimpa karama hii ndugu yetu na rafiki yetu R.Kelly ambaye ni maarufu sana hapa duniani kwa uimbaji wake. R. Kelly kabla hajaokolewa na damu ya Yesu Kristo alikuwa ni mwimbaji wa nyimbo za kidunia na alimtumikia shetani kwa muda mrefu sana na kuwapotosha walio wengi kutokana na uimbaji wake na sauti yake. Mungu alimfungua upofu wa kutotambua kuwa kile alichokuwa akifanya sio kizuri, akamuwezesha kumuokoa katika upofu huo na kumpa taa yenye mwanga mzuri wa Mungu. R. Kelly aliamua kuokoka na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na alifanya vizuri sana na kuwavuta walio wengi kwa kupitia nyimbo zake. Kama ilivyokawaida ya Mungu wetu, huwa hapendi kumbana mtu katika maamuzi yake, humwacha mtu kuamua kufanya lililo jema au baya na pale atakapokuwa ametambua ya kuwa amefanya baya Mungu hufungua tena milango yake na kumkaribisha muovu huyu kuingia na kujisafisha. Hii ilifanyika kwa ndugu yetu R. Kelly ambapo aliamua kuacha na wokovu na kuanza tena maisha ya kumtumikia shetani kwa njia ya uimbaji. Nyimbo zake zimekuwa na mvuto mkubwa sana duniani ambapo ukisikiliza utasikia na juu ya mapenzi na ukiangali video zao huwatumia wadada wakiwa nusu uchi na pia hupenda sana kutumia sigara na pombe katika video zake, na haya yote Mungu hapendi. Watu wengi duniani wamevutwa sana na kuiga maisha ya watu waoonyeshwa katika video zake. Hii ni mbaya sana na inasikitisha kuona watu wengi waangamia kwaajili ya mtu mmoja.

Huu ni wakati wa kumuombea ndugu yetu Robert Kelly kurudi tena kwa Mungu na kmtumikia MUNGU wetu. Ninaamimi akiokoka leo R.Kelly, watu wengi wataokoka kwani atakuwa ushuhuda mkubwa sana. Wachugaji,Manabii, Mitume, Waalimu, Wainjilisti, Mapadre, Waumini wote duniani tukiamua kupiga magoti hata kwa nusu saa kumuombea ndugu yetu arudi kundini, niaamini Mungu atasikia kilio chetu na kumrudisha mtumishi huyu kundini. Kumbukeni huyu alikuwa kondoo wa Mungu na sasa amepotea kwahiyo tunatakiwa kuwaacha hawa kondoo tuliokuwa nao kwa sasa kwasababu wako katika mkono salama na kumtafuta huyu kondoo mmoja aliyepotea.

Ukiangalia kwa makini sura ya R.Kelly katika picha yake ya kwanza utaona kabisa anachokifanya kinamsuta ndani ya mtima wake, na kuna picha nyingi ambayo wanatakiwa kaungalia watu wenye umri zaidi ya miaka 18 hapo chini, sura yake haiko sawa, nafsi yake inasema nooooooo!!!

Nduuuh, nimeongea sana ngoja nisepe kidogo ili utafakari niliyoyasema na Mungu akupe nguvu ya kusema jambo juu ya ndugu yetu na rafiki yetu R.Kelly.

Wko katika BWANA
Rulea Sanga,
www.rumaafrica.blogspot.com


Girlfriend wa Christiano Ronaldo, Irina Shayk akiwa katika pozi la uchi na msanii maarufu wa muziki wa R&B R. Kelly katika gazeti la V.Magazine. watu wengi wanajiuliza maswali kuhusiana na hali hii ya kumwamini R.Kelly na mwanamke, haswa msichana ambaye amekuwa na mwanasoka huyo maarufu kwa miaka zaidi ya mitano.
ANGALIA PICHA HII..NI KWA WENYE UMRI ZAIDI YA 18 TU...UONE SHTANI ANAVYOMTUMIA R.KELLY KUPOTOSHA WATU

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...