Monday, March 3, 2014

UZINDUZI WA ALBAMU YA MESS JACOB CHENGULA YA " MUNGU HABADILIKI" ULIOFANYIKA UBUNGO PLAZA SIKU YA JUMAPILI 02.03.2014


Siku ya Jumapili  ilikuwa ni siku ya furaha na ndelemo katika ukumbi tulivu wa Ubungo Plaza katika kukamilisha kusudi la Mungu juu ya mwimbaji maarufu Tanzania Mess Jacob Chengula alipokuwa akizindua albamu yake ya "Mungu Habadiliki" Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji zaidi ya 20 waliovamia jukwaa na kuwaacha watu kupagawa na uwepo wa Mungu ulioachiliwa kwa njia ya uimbaji. Viti vilikuwa havikaliki na kuwaacha  ma-MC kuwa katika wakati mgumu sana wa kuwaomba watu wakae chini.


Mh. January Makamba wa pili kutoka kushoto
Kila mwimbaji aliimba kwa kiwango cha juu sana mpaka mgeni rasmi Mh Januari Makamba kuwaita baadhi ya waimbaji ili ashikane nao mkono kama ishara ya ku-appreciate kazi yao, mmojawapo alikuwa Edson Mwasabwite.
Baada ya uimbaji kufanyika, mgeni rasmi akiongozana na wachungaji na wazee wa kanisa kutoka katika kanisa la Mito ya Baraka kwa Askofu Mwakiborwa anakoabudu Mess Jacob Chengula walipanda jukwaani kwa lengo zima la kuiombea albamu ile na kuifungua rasmi.
Mgeni rasmi Januari Makamba alipomaliza kuizindua aliweza kuongea machache kuhusiana na waimbaji. Aliwapongeza waimbaji kwa ushirikiano wao waliuonyesha katika kumuunga mkono rafiki yao Mess Jacob Chengula. Alikipongeza Chama Cha Muziki Tanzania na viongozi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kwa waimbaji wa nyimbo za Injili. Mh Januari Makamba aliwaalika viongozi wa Chama cha Muziki Tanzania na baadhi ya waimbaji kufika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili waweze kutoa matatizo yao na changamoto wanazopata katika huduma yao ya uimbaji.
Mh. Januari Makamba aliweza kuwaonya waimbaji wa nyimbo za injili juu ya style za uchezaji ambazo hazina baraka kwa mwenyezi Mungu kuziacha na kucheza kama vile Mungu anavyotaka watu wake wamchezee. Pia aliwaonya wale waimbaji ambao wamebarikiwa na kuwa maarufu sana, waachane na tabia ya kujivuna na kujiona wao ni wao. Mbali na kuwaalika katika Bunge, pia aliwaomba waimbaji na viongozi kutosita kufika ofisini kwake muda wowote na hakuna mtu atakayeweza kuwazuia kumuona hata kama atakuwa na majukumu mengi, lakini katika masuala ya Mungu kwa kupitia waimbaji na viongozi wa nyimbo za injili yuko tayari kusimamisha kwa muda na kuwasikiliza.
Wimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

MDOGO WAKE NA MH.JANUARI MAKAMBA AKITAMBULISHA WATU WALIONGOZANA NA KAKA YAKE MH.JANUARI MAKAMBA
 Mdogo wake na Mh. Januri Makamba
Mtoto wa Mh Januari Makamba akitambulishwa
Mh Januari Makamba akimwangalia mwanae wakati wa kutambulishwa
 Mtangaza wa Passion FM Bwana Sanga

KIPINDI CHA WAIMBAJI KUACHIA MASONGI YA BWANA MUNGU WETU
Silas Mbise
 Neema Gasper

KIPINDI CHA MESS JACOB CHENGULA KUINGIA UKUMBINI KWA MARA YA KWANZA

Mess Jacob Chengula akiongozana na Masanja Mkandamizaji wakiingia ukumbini
Watu wakimsindikiza Mess Jacob Chengula akielekea kwa Mgeni Rasmi Mh. Januari Makamba

Mh. Januari Makamba akisalimiana na baadhi ya waimbaji akiwemo Masanja Mkandamizaji, Bony Mwaitege na wengine wengi waliomsindikiza Mess Jacob Chengula katika High Table
Mess Jacob Chengula akisalimina na mdogo wake na Mh. Januari Makamba na kulia ni mwanae na mheshimiwa
Bony Mwaitege


Kulia ni Mess kabla ya kuzindua albamu yake akiwa katika pozi baada ya kumaliza zoezi la kuwasalimia wageni waalikwa waliokaa katika High Table ya Mh. Janauari Makamba
Hawa ni waimbaji wa nyimbo za Injili waliokaa High Table
 Mess Jacob Chengula akisalimiana na Mgeni Rasmi Mh. Januari Makamba
 Mess Jacob Chengula na Mh. Januari Makamba

 Masanja Mkandamizaji na Bony Mwaitege
Mh. Januari Makamba akicheza wakati Masanja Mkandamizaji akilianzisha songi lake la Watu wako Biszeee


KIPINDI CHA KUSOMA RISALA YA MESS JACOB CHENGULA
 John Shabani akisoma hotuba ya Mess jacob Chengula kwa mgeni Rasmi Januari Makamba

John Shabani

John Shabani akimkabidh mgeni rasmi Mh Januari Makamba hotuba ya Mess Jacob Chengula

Mh Januari Makamba aweka saini katika hotuba ya Mess Jacob Chengula
 Neema Gasper aliamua kutokelezea baada ya ku-perform
Neema Gasper
Tiketi zilizotumika katika uzinduzi huu. Kazi imefanywa na RumAfrica +255 715 851523

Picha zimepigwa na RumAfrica
+255 715 851523
Tembelea
SEHEMU YA TATU ITAKUUJIA MUDA SI MREFU, ENDELEA KUFUATILIA KATIKA BLOGU YETU HII

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...