Thursday, March 13, 2014

BIRTHDAI YA BONGO MOVIE KUDHAMINIWA NA WINDOEK


Mzee Chillo na Wolper wakibadilishana mawazo.
MABIBO beer, wines and spirits Ltd, waaagizaji na wasambazaji wa kinywaji cha Windhoek Tanzania, ndiyo mdhamini mkuu wa maadhimisho ya kutimiza miaka mitatu ya Bongo Movies yanayotarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu.

Mdhamini huyo ametambulishwa leo na Mwenyekiti wa Bongo Movies, Steve Nyerere katika ukumbi uliopo ndani ya jengo la Arcade, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi kwenye ofisi hizo, Steve baada ya kumtambulisha mdhamini huyo, alisema kuwa wamepania kufanya mambo makubwa siku hiyo kwani kutakuwa na uchaguzi wa balozi wa kinywaji hicho kimataifa pamoja na utoaji tuzo za heshima kwa waliotangulia mbele ya haki.

Aidha aliongeza kuwa, siku hiyo kutakuwa na wasanii mbalimbali watakaosindikiza maadhimisho hayo wakiwemo Banana Zorro, Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma na wengine wengi huku kiingilio kikiwa shilling 10,000/= Viti vya kawaida na 50,000/= kwa VIP.
Tiketi za maadhimisho hayo zitaanza kuuzwa siku tatu kabla kwenye Klabu ya East 24 iliyopo Mikocheni B, Dar.
Viongozi wa Bongo Muvi Steve Nyerere, Cloud na William Mtitu katika pozi.
Mama Rolaa akipata msosi kwenye utambulisho huo.
 
Wastara naye alikuwepo.


POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...