Sunday, February 23, 2014

AC MILAN YAIPIGA BAO SAMPDORI 2-0

AC Milan imeendelea kujikongoja kwenye Ligi Kuu ya Seria A baada ya jioni hii kupata ushindi wa pili mfululizo kwa kuilaza Sampdoria nyumbani kwao kwa mabao 2-0.
Adel Taarabt alianza kuiandikia Milan bao la kwanza katika dakika ya 12 bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.Kipindi cha pili vijana wa Clarence Seedorf waliingia kwa kasi na kupata bao la pili lililofungwa na Adil Rami kwenye dakika ya 58, huku Sampdoria ikimpoteza Lopez aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano na kufuatiwa na nyekundu.

Ushindi huo umeifanya Milan kufikisha pointi 35 na kubaki nafasi ya 9 ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Juventus inayotarajia kushuka dimbani muda mchache kuvaana na Torino.

Adel Taarabt

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...