Sunday, February 23, 2014

MTANGAZAJI WA WAPO RADIO FM SILAS MBISE NA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA MESS JACOB CHENGULA WATETA JUU YA TAMASHA LA UZINDUZI WA ALBAMU YA MUNGU HABADILIKI


Zikiwa zimebaki siku chache kufikia Machi 02, 2014 wtu wa Mungu kujumuika kwa pamoja katika eneo la kujidai kwa Yesu la Ubungo Plaza katika kuzindua albamu yenye ujumbe wa Mungu kwaajili yako ya MUNGU HABADILIKI, Mess Jacob Chengula aliwasha gari lake na kuchoma mafuta yake mpaka katika kituo cha utangazaji cha WAPO  radio ambapo aliweza kukutana na mtangazaji wa WAPO Radio Silas Mbise na kujificha katika kona moja wakiteta juu ya ujio mpya wa uimbaji.


Kulia ni Silas Mbise akiwa na Mess Jacob Chengula katika kituo cha utangazaji WAPO Radio FM Kurasini

Mess Jacob Chengula aliamua kufunguka na kuwajuza watu wa Mungu waliokuwa wakisikiliza WAPO radio kufika bila ya kukosa katika kumtukuza Mungu siku ya Jumapili 02/03/2014 katika ukumbi wa UBUNGO Plaza saa sita mchana.

Waimbaji zaidi ya 20 wataimba siku hiyo wakati mgeni rasmi Mh Januari Makamba atakuwa ndani wa mjengo akimsifu Mungu. USIKOSE SIKU HIYO kwani kiingilio ni Tsh 5000 viti vya Mtanzania wa kawaida na VIP ni Tsh 10,000 tu

Tangazo limetengezwa na RumAfrica
+255 715 851523

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...