Thursday, August 29, 2013

ALIYEMPASUA AUNT EZEKIEL NI HUYU HAPA


 
Mrembo Yvonne aliyempasua kwa chupa Aunt Ezekiel usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas Posta jijini Dar es Salaam.

MREMBO aliyempasua mwigizaji wa sinema za Bongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ ajulikanaye kwa jina la Yvonne. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, ambapo Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto. 
 Vurugu kubwa ilizuka baada ya tukio hilo na Aunt alikimbizwa hospitali ya Aga Khan huku Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.
 
Mkono wa Aunt Ezekiel  uliopasuliwa na Yvonne kwa chupa.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...