Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWS: ASKOFU MOSES KULOLA WA KANISA LA E.A.G.T AFARIKI DUNIA


 
Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake.

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi, Moses Kulola amefariki dunia leo hii.
Habari hizi zimethibitishwa na mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya, Mch. Daniel Moses Kulola kupitia katika akaunti yake ya Facebook. kwa kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU." 

Hivi karibuni marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch. Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa baada ya kupata nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...