Thursday, July 11, 2013

SIPO TAYARI TENA KUMVULIA NGUO MR. BOND.".....AUNT LULU


Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amesema yeye na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Salim imebaki historia na kamwe hawawezi kurudiana naye japo anayajua mapenzi.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema ameshaamua kujituliza kwa mpenzi wake wa sasa hivyo hata iweje hawezi kurudiana na Bond.

“Jamani kwa sasa mnaona nimebadili kabisa staili ya maisha yangu hivyo Bond atabaki kuwa rafiki kama walivyo marafiki zangu wengine.

“Niliwahi kuachana naye kipindi flani baadaye tukarudiana kutokana na ukweli kwamba ni mwanaume anayejua kupenda na anayajua mapenzi ,lakini hii ya sasa ndiyo imetoka, kamwe siwezi kurudiana naye,” alisema Aunty Lulu.

1 comment:

  1. Jamanieee mwambieni Aunty Lulu kwambwa nipo tayari kwa kumutia ndani ya yumba baada ya kuachana na Bond Bin S. email yangu hii:halindintwar@yahoo.com

    ReplyDelete

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...