Thursday, July 11, 2013

MFANYA BIASHARA NDOGONDOGO ATANGAZWA MSHINDI WA DROO YA TATU YA WINDA NA USHINDE YA BIA YA SERENGETI



Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde ambaye ni Bi Blanca Mariki, katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na wadau wengine wa droo hiyo Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko (kushoto).
 
Mfanya biashara ndogondogo kutoka Morogoro atangazwa mshindi wa kitia cha 1,000,000 kutoka kampuni ya bia ya Serengeti kwa promosheni hiyo.
11 Julai 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa droo ya mwisho ya promosheni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya tatu na ya mwisho. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi yamichezo ya Bahati Nasibu.

Baada ya kupokea simu Blanca Mordest Mariki(30) anayefanya biashara ndogo ndogo kutoka Morogoro alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nimefurahi sana kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya Bia ya Serengeti. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya” Pamoja na ushindi huu mkubwa nimeshajishindia bia za bure za Serengeti mara mbili, pamoja na hela taslimu shilingi 10,000 mara nne ambazo huwa natumiwa kupitia njia ya simu”. Alisema mshindi huyo.

Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watanzania wengi wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100,000/= na pia washindi wetu wakubwa wa droo ya kwanza na ya pili walijishindia milioni moja kila mmoja. Mshindi wa droo ya kwanza alitoka Kilimanjaro na mshindi wa pili alitoka Dar es Salaam na wote waliipongeza sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwasaidia wateja kwani wameinua uchumi wao kupitia ushindi wao wa promosheni hii”.

“Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wao kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bia yetu ya Serengeti. Promosheni hii inaendelea mpaka mwisho wa mwezi Julai na kumalizika kwa promosheni ya Winda na Ushinde ni mwanzo wa mengine mengi yanayotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ajili ya wateja wetu”. Aliongeza meneja huyo.

Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiongea na mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde kwa njia ya simu, huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Tanzania Emmanuel Ndaki(wa kwanza kushoto), Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(wa pili kushoto) na Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia), katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.

Allan Chonjo ambaye ni Meneja wa bia ya Serengeti akiongea na Blanca Mariki(mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde) kwa njia ya simu katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam.

Akitoa maelezo kwa wana habari kuhusiana na droo ya tatu ya Winda na Ushinde Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo akiwa na wadau wengine walioshiriki katika droo hiyo jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...